honour

(US honor) n 1 heshima, utukufu, adhama show ~ to one's parents heshimu, onyesha heshima kwa wazazi. do somebody ~; do ~ to somebody toa heshima/ heshimu mtu. maid of ~ n mpambe (hasa wa malkia) guard of ~ gwaride la heshima. 2 sifa njema; uaminifu; uadilifu. on one's ~ kwa sifa/uaminifu wake. an affair of ~ (hist) pambano la kutetea hadhi. be/feel (in) ~ bound to do something wajibika (sio kwa sheria). one's word of ~ ahadi, kutimiza jambo. pay/incur a debt of ~ lipa deni kwa heshima. put somebody on his ~ amini mtu. 3 (in polite formulas) kuheshimu, kustahi (mtu). do somebody the ~ of fanyia mtu heshima. have the ~ of/to -wa na heshima ya (formal style) I have the ~to write to you nina heshima kukuandikia. 4 Your/His ~ Mheshimiwa, Mtukufu. 5 an ~ n mtu/jambo lenye kuleta sifa she is an ~to her group yeye ni mfano mzuri kwa kikundi chake. 6 (pl) maadhimisho ya heshima, cheo, nishani. full military ~ n heshima zote za kijeshi (agh. kwa mazishi ya shujaa au kukaribisha kiongozi wa heshima). do the ~s (colloq) (of the table,house etc.) karibisha. 7 (pl) (in universities) nafasi ya juu katika digrii. ~s degree n digrii ya daraja la juu. 8 (in card games) karata ya thamani kubwa. vt 1 heshimu, tukuza, adhimu. 2 (comm) pokea na lipa kwa wakati maalum ~ a debt lipa deni ~ one's signature kiri/kubali sahihi na kulipa fedha. honorary adj 1 (shortened in writing to Hon) (of a position) -sio na malipo the honorary secretary katibu asiyelipwa. 2 (of a degree, rank) -a heshima an honorary member mjumbe wa heshima. honorarium n honoraria, tunzo (isiyodaiwa). honorific adj (of expression) -a heshima. ~ able (US honorable) adj 1 -a heshima, tukufu ~able burial mazishi ya heshima. 2 honourable (abbr. Hon) Mheshimiwa. Right ~able (abbr. Rt Hon) jina la heshima kwa wenye vyeo maalum k.m. waziri n.k. honourably adv.