hold

hold

1 vt,vi 1 shika, kamata. ~oneself well jiweka imara; simama vizuri. ~ the line shikilia simu. 2 zuia. ~ one's breath zuia pumzi (kwa woga n.k.). ~ one's fire acha kupiga risasi kwa muda. ~ one's tongue/peace nyamaza, kaa kimya. there is no ~ing somebody/ something haizuiliki, haiwezekani kumzuia/kuzuia. 3 shikilia. ~ oneself in readiness (for) jitayarishe (kwa hatari), kaa tayari (kwa dharura). ~ one's sides with laughter shikilia mbavu, cheka sana/vunjika mbavu. 4 weka; -wa na uwezo wa kuweka; chukua this tank ~s 30 litres tangi hili linaweza kuweka lita 30. (not) ~ water (isiyo) kubalika. ~ something in one's head kumbuka. 5 fanya watu wasikilize, sisimua the speaker held his audience spellbound msemaji aliwasisimua wasikilizaji wake. 6 ona; chukulia, amini. ~ somebody in high/low esteem heshimu/dharau mtu. ~ something dear/cheap kuza/shusha thamani ya kitu, thamini sana/ kidogo. 7 linda; shikilia. ~ the fort (fig) -wa na madaraka mwenyewe anapoondoka. ~ one's ground simama tisti. ~ one's own kacha, -torudi nyuma. 8 fanya, anzisha, endesha ~ a meeting fanya mkutano. ~ court (fig) karibisha, starehesha, kubali kuwa na maongezi na (washabiki/ wapenzi). 9 -wa na haki ya, miliki. 10 -endelea vizuri. 11 shika nafasi. office ~er n mwenye ofisi. 12 himili, beba the new car ~s the road well gari hili jipya linahimili barabara. 13 (uses with adverbial particles and preps). ~ something against acha kitu kiathiri wazo la mtu don't ~ his political views against him usimchukulie kuwa na makosa kwa sababu ya mawazo/ msimamo wake kisiasa. ~ back sita. ~ somebody/something back fanya mtu/kitu kisite; zuia; (of secret) ficha. ~somebody/ something down shikilia; kandamiza. ~ a job down (colloq) dumu kazini (kwa kuonyesha uwezo). ~ forth sema kwa kujikweza; jigamba; hubiri. ~ something forth toa; pendekeza. ~ something in zuia ~ in one's temper jizuia (hasira). ~ off jitenga, kaa/baki mbali; chelewesha. ~ somebody/ something off zuia mtu/kitu mbali. ~ on simama imara (kwenye matatizo/hatari); (usu imper) acha ~ on a minute acha kwanza kidogo! ~ on to shikilia; -tokubali kutoa mali n.k.. ~ something on shikilia; weka bolts and nuts ~ the wheels on parafujo na nati hizi vinashikilia magurudumu mahali pake. ~ out shikilia; -tojisalimisha; dumu, endela kuwepo; (of hand) nyosha the workers are still ~ing out for higher wages wafanyakazi bado wanaendelea kudai mishahara ya juu. ~ out on kataa kupatana/ kushirikiana. ~ somebody/ something out wa na mtu/kitu; toa. ~ something over ahirisha. ~ something over somebody tumia kitu kutisha; tishia. ~ to something fanya mtu atimize ahadi/mkataba, shikilia kuwa mwaminifu kwa; endelea kushikilia. ~ somebody to something fanya mtu aweke ahadi n.k.. ~ somebody (up) to ransom shikilia mtu mateka (ili kudai vitu mbalimbali). ~ together shikamana. ~ somebody/ something together fanya ishikamane. ~ somebody/ something up shika, zuia; chelewesha; shikilia kwa nguvu/vitisho (ili kuibia n.k.). ~ up n ushikiliaji wa nguvu, wizi; fanya kuwa mfano. ~ somebody up to derision/scorn/ ridicule dhihaki mtu. ~ with something kubali.

hold

2 n 1 mshiko; kushika; uwezo wa kushika. 2 amri, madaraka he has great ~ over him ana madaraka makubwa juu yake. 3 mahali pa kushikia. 4 (boxing and wrestling) mashiko. holdall n begi kubwa la kubebea nguo. holder n 1 kishikizi, kishikilia. 2 mwenye madaraka; mpangaji; mmiliki; mshikaji. holding n kiwanja, shamba; umilikaji (agh wa ardhi). small ~ ing n shamba dogo. ~ing company n kampuni mama.

hold

3 n sehemu ya meli ya kuwekea mizigo.