high

adj 1 -juu, -refu (kwa kwenda juu) The clouds are ~ in the sky mawingu yako juu angani Kilimanjaro is the ~est mountain in Africa Kilimanjaro ndio mlima mrefu kabisa barani Afrika. ~ and dry adj (of a ship) -liokwama; nje ya maji; (fig) -liopitwa na wakati, -liotelekezwa, -liotengwa. (do something) with a ~ hand fanya jambo kwa kiburi. 2 -kuu, -a juu; muhimu. a ~ official n afisa wa cheo cha juu ~ society tabaka la juu. the Most ~ (in the Bible) Mungu. ~ and low watu wa matabaka yote katika jumuia, watu wote. 3 (of sounds) kali; -a kidato cha juu speak in ~ tone ongea kwa sauti kali ya kidato cha juu. 4 -a juu; kali; kubwa. ~ prices n bei kubwa/ya juu. ~ words n maneno makali. ~ living n maisha ya juu; anasa. 5 ~ time n wakati wa kufanya jambo it is ~ time you left wakati wa kuondoka umewadia, afadhali ufunge virago! 6 -enye heshima, ema, adili(fu) a girl of ~ character msichana mwenye tabia njema. ~ ideals n maadili mema. 7 H~ Church n Kanisa la Anglikana la UMCA (ambalo huwapa maaskofu na mapadri mamlaka ya kutoa sakramenti). H~-Churchman n muumini wa kanisa. 8 (of food esp. meat and game) -liovunda. 9 (colloq) -liolewa, -levi. 10 (colloq) -liolewa bangi/madawa. 11 n kiwango cha juu. from (on) ~ kutoka mbinguni the income reached a new ~ this year mapato yalifikia kiwango cha juu mwaka huu. 12 (compounds) ~ ball n (US) pombe kali na soda au maji (ndani ya glasi ndefu). ~est bidder n mzabuni wa juu. ~ born adj -a uzao bora, hababuu. highboy n (US) kabati refu lenye saraka. highbrow n, adj (person) -enye (mambo) makuu (agh. hutumiwa kwa kudharau). ~ chair n kiti kirefu cha mtoto. high-class adj daraja la kwanza/juu. ~ colour n (of complexion) rangi nyekundu iliyokolea. H~ Commissioner n Balozi wa nchi ya Jumuia ya Madola katika nchi nyingine ya Jumuiya ya Madola. ~ Court n Mahakama Kuu. ~ day n (only in) ~ days and holidays sikukuu. ~ explosive n baruti kali yenye mshindo mkubwa. ~ falutin adj (colloq) -a mbwembwe. ~ fidelity n. adj (abbr.hi-fi) (of radios, records, tapes etc) -enye kutoa sauti safi. ~-flier;flyer n mtu mwenye tamaa kubwa ya kufanikiwa katika maisha. ~ flown adj -enye makeke, -enye majisifu/ mbwembwe. ~ flying adj (fig) (of persons) -enye tamaa sana. ~ frequency n (abbr. hf) -a masafa marefu. H~ German n Kijerumani sanifu. high-grade adj -a daraja ya juu. high-handed adj onevu, -dhalimu. high-handedly adv. highhat adj, n fidhuli, -enye makuu. vt dharau, dhalilisha. the ~ jump n kuruka juu. be for the ~ jump (sl) stahili adhabu kali you'll be for the ~ jump utaipata, utakiona. ~ keyed adj (of sound) kali; (fig) -enye mpapatiko. highland n milimani, uwanda wa juu. high-level adj (attrib only) (of conferences etc) -a ngazi ya juu. ~ life n (a) maisha ya kisasa na ya anasa (in W. Africa) hailaifu: mtindo wa muziki na dansi. ~ light n (usu pl) sehemu ya picha yenye kuakisi wanga; (fig) sehemu yenye kuvutia au kuonekana waziwazi vt sisitizia; -pa umuhimu. ~ Mass n (in R.C. Church) Misa kuu. high-minded adj -enye msimamo, -enye maadili. high-mindedly adv. high-mindedness n. high-necked adj (of a dress) -a kukaba roho. high-pitched adj (of sounds) -kali, (of roof) -a paa -liochongoka. high-powered adj -enye juhudi, -enye nguvu nyingi. high-pressure n kanieneo ya juu; (fig) shupavu, -enye juhudi. high-priced adj ghali. ~ priest n kuhani mkuu. high-principled adj -enye msimamo, nyofu. high-ranking n adj (of officers) -enye cheo cha juu. ~ rise adj maghohorofa marefu. highroad n barabara kuu, (fig) njia ya moja kwa moja. H~ school n sekondari ya juu. the ~ seas n bahari kuu. ~- sounding adj (of style) -enye kuvutia; -a mbwembwe. high-spirited adj changamfu, -epesi, kunjufu; (of a horse) -enye kwenda mbio. ~ spot n tukio muhimu. ~ street n barabara kuu/muhimu (katika mji). ~ table n meza kuu. ~ tea n mchanganyiko wa chai na chakula cha jioni. high-tension adj (electric) -enye volteji kubwa. ~ tide n maji kujaa, maji makuu. ~ toned adj -a juu (katika jamii au kisomo). ~ treason n uhaini. ~ up n (colloq) mtu mashuhuri; mtu wa cheo cha juu. ~ water n see ~tide. ~-water mark n alama yenye kuonyesha kikomo cha juu cha maji kujaa; (fig) upeo wa mafanikio. highway n; ~ road barabara kuu. H~ way Code n kanuni/sheria za barabara. ~-way-man n haramia, mnyang'anyi adv juu (lit,fig) lipa bei kubwa. live ~ ishi kitajiri (kwa vinono na vinywaji kochokocho). fly ~ (fig) -wa na tamaa kubwa. hold one's head ~ jiamini, jiona. run ~ (of the sea) kabiliwa na mkondo mkali na maji makuu; (of the feelings) chacharika. search/look/hunt ~ and low (for something) tafuta kila mahali. highly adv sana he spoke ~ ly of her alimsifu sana. ~ ness n 1 (opposite of lowness) hali/sifa ya juu. 2 (title) Mstahiki, mtukufu.