heart

n 1 moyo ~ attack shtuko la moyo. 2 kiini cha hisia, (hususa mapenzi) undani wa tabia ya mtu a man with a kind ~ mtu mwenye roho nzuri/huruma. after one's own~ -enye kupendeza nafsi; -a kuafikiana. at ~ kimoyomoyo, kwa kweli; kimsingi. have something at ~ penda moyoni, vutiwa/pendezewa na. from (the bottom of) one's ~ kwa yakini, kwa dhati. in one's ~ of ~s moyoni. to one's ~'s content kiasi chake. with all one's ~ kwa utashi/moyo wote I love you with all my ~ nakupenda kwa moyo wangu wote. ~ and soul kabisa I am yours ~ and soul mimi ni wako wa daima break a person's ~ vunja moyo; sikitisha. cry one's ~ out wazia sana (agh kwa siri). do one's ~ good tia moyo. get/learn/know something by ~ kariri. have a ~onyesha huruma. have a change of ~ badilisha mawazo/msimamo. have the ~ to (usu neg) -wa na moyo mgumu, -tokuwa na huruma. have one's ~ in something vutiwa/pendezewa na kitu. have one's ~ in one's boots katishwa tamaa sana. have one's ~ in one's mouth ogopa sana. have one's heart in the right place -wa na moyo mzuri; -wa mkweli. have one's ~ set on something taka sana. lose ~ kata tamaa. lose one's ~ to somebody/something penda sana mtu/kitu. set one's ~ on something/having something/doing something etc taka sana; -wa na shauku kupata/kufanya kitu. take (fresh) ~ (at something) jiamini. take something to ~ athiriwa na jambo. wear one's ~ on/upon one's sleeve onyesha hisia kwa uwazi. 3 katikati ya (kitu); kiini (cha jambo) in the ~ of the forest katikati ya msitu the ~ of the matter kiini cha jambo. 4 (of land) rutuba in good ~ katika hali nzuri out of ~ katika hali mbaya. 5 (cards) kopa. 6 (as a term of endearment to a person) dear ~ mpenzi sweet ~ mpenzi. 7 (compounds) heartache n huzuni kubwa. heartbeat n pigo la moyo. ~ breaking adj -a kuhuzunisha sana; -a kuvunja moyo. ~ broken adj -enye huzuni nyingi. heartburn n kiungulia. ~ burning n kijicho. ~ disease n afkani, ugonjwa wa moyo. ~-failure n moyo kusita/ kufa. heartfelt adj -a dhati. ~ rending adj -a kuhuzunisha sana. heartsick adj -enye huzuni, -enye kusononeka. ~ strings n upendo, mapenzi. hearted adj (in compounds) hard ~ -enye moyo mgumu faint-~ -oga. heartless adj -katili; -sio na huruma. heart-searching n -kujichunguza. heartlessly adv. heartlessness n. hearten vt tia moyo; changamsha. hearty adj 1 -a kweli, kunjufu. 2 zima, -enye nguvu, -enye afya njema. heartily adv 1 kwa nia njema, kwa hamu. 2 sana I am ~ily glad that you sent me a letter nimefurahi sana kwamba umeniletea barua. heartening news n habari za kutia moyo/ kuchangamsha.