head

n 1 kichwa; (fig) maisha it costed him his ~ amepoteza maisha yake. 2 kipimo cha kichwa ~'s length urefu wa kichwa John is taller than Mary by a ~ John amempita Mary urefu kwa kichwa. be ~ and shoulders above somebody (fig) pata/zidi sana (kwa uwezo au akili). 3 ~ (s) upande wa sarafu wenye kichwa. ~s or tails? Kichwa au Mwenge? be unable to make ~ or tail of something -toweza kuelewa kitu. 4 mtu the entrance fee is 200/= per ~ kiingilio ni Shs 200/= kwa kila mtu. 5 (pl unchanged) moja katika kundi, idadi fifty ~ of sheep kundi la kondoo hamsini. 6 akili; uwezo wa kufikiri he made it up out of his own ~ alitunga mwenyewe. 7 kipaji he has a good ~ for leadership ana kipaji cha uongozi. 8 (kitu kama) kichwa (kwa umbo, kazi au mahali) the ~ of a nail kichwa cha msumari the ~ of a hammer kichwa cha nyundo. 9 sehemu ya juu/mwanzo at the ~ of the list mwanzoni mwa orodha. 10 sehemu ya juu/ya mwisho wa kitu the ~ of a bed kichwani mwa kitanda. 11 (of plants) kishada cha majani au maua juu ya shina a ~ of cabbage kabeji. 12 (often attrib) mtawala, mkuu, kiongozi the ~ of the school mkuu wa shule crowned ~s mfalme na malkia. H~ of State n Mkuu wa Nchi. 13 sehemu ya mbele (of a ship) omo at the ~ of a queue mwanzo/mbele ya mlolongo/foleni at the ~ of a ship omoni. 14 (chiefly in proper names) rasi. 15 kiasi cha maji kinachowekwa kwa sababu maalumu (k.m. ya kuzalisha nguvu za umeme) ~ of a steam nguvu ya mvuke. 16 kichwa cha habari this essay has several ~s insha hii ina vichwa vya habari kadhaa. 17 povu (agh. la maziwa, pombe n.k.). 18 ncha/mdomo/kichwa cha jipu (lililoiva) the boil came to a ~ jipu liliiva. come to a ~ (fig) iva; fikia upeo (wa hatari) misunderstanding has come to a ~ kutoelewana kumefikia hatua ya hatari. 19 (various phrases) above/over one's ~ ngumu kuelewa. talk above their ~s ongea pasipo kueleweka. an old ~ on young shoulders busara aliyonayo kijana. bite somebody's ~ off kemea kwa hasira; jibu vikali. eat one's ~ off (of a horse) kula sana (na fanya kazi kidogo). give somebody his ~ ruhusu mtu afanye atakavyo. go to one's ~ (of liquor) levya; lewesha, tia kiburi/majivuno. have a good ~ on one's shoulder -wa na uwezo wa kutenda/busara. ~ over heels kichwangomba; (fig) kabisa keep one's ~ tulia. keep one's ~ above water (fig) epuka madeni/matatizo n.k. keep one's ~ down epuka hatari/uharibifu. laugh/scream one's ~ off cheka/lia kwa nguvu sana. lose one's ~ changanyikiwa! (go) off one's ~ pata wazimu. (stand etc) on one's ~ simama kichwangomba I could do it (standing) on my ~ (colloq) ni rahisi mno; hainipi shida. on one's own ~ be it shauri hako. over one's ~; above one's ~/over another's ~/over the ~s of others mbele ya mtu/watu waliotangulia/stahili zaidi. put our/your/their ~s together shauriana. put something into a person's ~ endekeza/ shauri mtu. put something out of one's ~ sahau, acha kufikiria, acha wazo fulani. put something out of somebody's ~ sahaulisha. take something into one's ~ amini kitu fulani. talk one's ~ off zungumza kupita kiasi. talk somebody's ~ off chosha (mtu) kwa maongezi. two ~s are better than one (prov) penye wengi hapaharibiki neno. turn somebody's ~ pumbaza, tia kiburi; lewesha ajivune. (be) weak in the ~ pungukiwa na akili. 20 (compounds) ~ ache n maumivu ya kichwa; (sl) tatizo, shida it gives me a ~ache inanisumbua akili. ~ band n utepe/ukanda wa kichwa. ~ dress n ukaya, dusumali, kilemba. ~ gear n kofia, chepeo. ~ hunter n muuaji anayehifadhi vichwa vya maadui zake; (fig) mtu anayeshawishi kwa nguvu ujiunge na shirika, jeshi n.k. ~ lamp/light n taa ya mbele (ya gari, meli n.k.). ~ land n rasi. ~ line n kichwa cha habari (pl) habari kwa ufupi (agh katika radio). headman n (pl men) mjumbe. ~ master n mkuu wa shule (mwanamume). headmistress n mkuu wa shule (mwanamke). ~ on adj, adv (of collisions) uso kwa uso. headphones n pl vipokea sauti vinavyobanwa kichwani. headpiece n kofia ya chuma; (colloq) bongo, akili. headquarters n (sing or pl) makao makuu. ~ rest n msamilo. headroom n nafasi. ~ set n see ~ phones. headship n ukuu (agh. wa shule). headstall n sehemu ya hatamu inayovishwa kichwani. ~ stone n jiwe linalowekwa kichwani mwa kaburi. ~ wind n upepo wa mbisho. headword n kitomeo. headed adj (in compounds) -enye kichwa three ~ed -enye vichwa vitatu long ~ed -enye kichwa kikubwa. headless adj -sio na kichwa. vt,vi 1 ongoza Kimathi ~ed Mau Mau Kimathi aliongoza Mau Mau. 2 -wa juu/ mwanzo. 3 gonga kwa kichwa, piga kichwa. 4 ~something/somebody off badilisha mwelekeo; rudisha (fig) zuia. header n 1 kuanguka/ kupiga mbizi kwa kutanguliza kichwa. 2 (football) kupiga mpira kwa kichwa. heading n kichwa cha habari. headlong adv,adj 1 -a kutanguliza kichwa fall ~long anguka kwa kutanguliza kichwa. 2 -a ubahau, bila kufikiri a ~long decision uamuzi bahau. headstrong adj -kaidi, -bishi. heady adj (of alcoholic drink) -a kulevya haraka.