hay

n nyasi kavu. make ~ kausha nyasi, geuza nyasi (ili zikauke). make ~ of vuruga. make ~ while the sun shines linalowezekana leo lisingoje kesho, tumia nafasi iliyopo. ~ cock n tita la nyasi kavu shambani. ~ fever n kikohozi/mafua yaletwayo na vumbi. ~ fork n uma wa kubebea nyasi kavu shambani. ~ loft n ghala ya nyasi kavu. haymaker n mkausha nyasi. ~ making n kukausha nyasi. hayrick; ~ stack n lundo la nyasi (lililofungwa tayari kuhifadhiwa ghalani). ~ wire n waya wa kufungia marobota ya nyasi kavu pred adj (colloq) -lio ovyo ovyo/ vurugika; -enye wasiwasi/ hamaniko, fadhaa/wazimu. go ~wire (of persons) hangaika, hamanika, pata wazimu; (of something e.g a plan) vurugika.