hang

n 1 (sing only) mning'inio, mkao the ~ of a dress mning'inio wa gauni. 2 get the ~ of something (colloq) elewa jinsi ya kutumia (teknolojia, mashine, wazo n.k.); pata/ona maana au umuhimu wa kilichosemwa au kuandikwa. not give/care a ~ (colloq) (euph for damn) -tojali chochote. vt,vi 1 tundika, angika, ning'iniza, ngoeka ~ the pictures on the wall tundika picha ukutani ~ the towel on the line angika taulo kwenye kamba. 2 (pt, pp hanged) nyonga he ~ed himself alijinyonga he was ~ed for murder alinyongwa kwa kuua 3 (mild equivalent of damn-dated) I'll be ~ed if I come sitakuja kabisa; wallahi siji! 4 (various uses) ~ a door tia mlango bawaba. ~ by a hair/a single thread (of a person's fate) -wa katika hali mbaya/ngumu; tegemea kitu kidogo; wa mashakani sana. ~ one's head inamisha kichwa hasa kwa aibu. ~ fire (of a gun) kawia kufyatuka; (of events) kawia kutokea/kuanza. let things go~ (colloq) puuza, -tojali. ~ in the balance -wa na matokeo yenye mashaka, -wa mashakani. 5 acha leave ~ing until the right time acha mpaka wakati ufaao. 6 (compound) hangman n chakari, mnyongaji. ~ dog adj (of somebody's look) -danganyifu na -liotahayari; -enye aibu. hangover n kasumba; uchovu baada ya kulewa sana; mabaki ya habari; sheria za zamani; (with adverbial particles and preps) colonial ~ over kasumba ya kikoloni. ~ about/a round randaranda. ~ back sita. ~ on shikilia kwa nguvu; vumilia. ~ on (a minute) (colloq) ngoja kidogo. ~ on/upon somebody's words/lips sikiliza kwa makini. ~ on to something ng'ang'ania; shikilia imara. ~ out (sl) ishi; panga. ~ something out tundika, anika, angika (nguo mbichi) juani zikauke; onyesha. ~ together (of persons) saidiana; shirikiana if we dont ~ together we shall fail tusiposhirikiana tutashindwa; patana, lingana the evidence of the witnesses ~s together ushahidi wa mashahidi unalingana. ~ up kata simu. ~ up on somebody (colloq) kata simu kabla mtu mwingine hajamaliza kuongea. be hung up cheleweshwa; katishwa tamaa; fadhaika. hang-up n 1 shida, matatizo. 2 fadhaa. hanger n kiango (cha kutundikia vitu) (in compounds) clothes-/dress-~er kiango cha nguo. hanger-on n mtu anayejitiatia, mdoezi. hanging n 1 kufa kwa kunyongwa. 2 (usu.pl) pazia.