handle
n 1 mpini; (of a cup) mkono; (of a bucket) utambo; (of a door or box) kipete. ~ bar n (often pl of a bicycle) usukani. fly off the ~ (colloq) hamaki, pandisha. (fig) give a ~ (to somebody) (against somebody) toa nafasi, kisingizio kinachoweza kudhuru/kuumiza. 2 (sl) cheo; jina la heshima have a ~ to one's name -wa na jina la heshima k.m. Alhaji. vt 1 gusa, shika ~ the ball gusa mpira kwa mikono. 2 simamia; shughulika; ongoza, tawala. 3 (treat) tendea. 4 (comm) nunua; uza he does not ~ perishable goods in his shop hafanyi biashara ya bidhaa zinazoharibika upesi. handler n mtu afunzaye na kuwatunza wanyama k.m. mbwa wa polisi.