hand
hand
1 n 1 mkono, kitengele. at ~ karibu. at somebody's ~s kutoka kwa I did not expect such treatment at your ~s sikutarajia kitendo kama hicho kutoka kwako. bind somebody ~ and foot funga mikono na miguu; (lit. fig) zuia mtu asiweze kufanya chochote. serve/wait on somebody ~ and foot tumikia mtu sana. by ~ kwa mkono this sweater is made by ~ sweta hii imefumwa kwa mkono the letter was sent by ~ barua imepelekwa kwa mkono. bring up a baby/a calf by ~ lisha mtoto/ndama kwa chupa. eat/feed out of one's ~ (agh. ndege) fugika; (fig) -wa tayari kutii lolote. from ~ to ~ pokezana mkono kwa mkono. fight ~ to ~ pambana, pigana kwa kukaribiana sana. give/land (somebody) ~ (with something) saidia mtu. give one's ~ on a bargain kubaliana kwa kushikana mkono. have one's ~ full -wa na shughuli/kazi nyingi. ~ in ~ kwa kushikana mkono kwa mkono. (fig) H~s off! Acha! Usiguse! H~s up! Mikono juu! ~ over ~ kwa kutumia mikono yote; (fig) kwa haraka na uthabiti. in ~ tayari, mkononi cash in ~ fedha taslimu; (of work etc.) -nayoshughulikiwa. the matter is in ~ jambo linashughulikiwa. in the ~s of mikononi mwa; juu ya the matter is in your ~s ni juu yako. in good ~s salama, inayotunzwa vizuri the child is in good ~s mtoto anatunzwa vizuri. not lift a ~; not do a ~'s turn -tosaidia kabisa. lift/raise a/one's ~ against somebody tishia, shambulia. live from ~ to mouth ishi maisha ya kijungumeko; -wa maskini. (get something) off one's~s jitoa (katika wajibu); achana na. on ~ -liopo. on one's ~ chini ya madaraka ya; mikononi mwa. out of ~ -sioweza kudhibitiwa the crowd was out of ~ umati ulikuwa haudhibitiki. shake ~s (with) shikana mikono. take a ~ (in) saidia, shiriki. take something/somebody in ~ chukua madaraka ya. be to ~ (commerce) pokelewa your letter is to ~ barua yako imepokelewa. wash one's ~s of nawa mikono, jitenga na. win ~s down shinda kwa urahisi. (rule) with a heavy ~ (tawala) kwa ukali. win a lady's ~ kubaliwa uchumba. 2 (pl) uwezo, mamlaka, madaraka. in somebody's ~s chini ya madaraka ya mtu fulani the house is no longer in my ~s sina madaraka tena. change ~s badili umiliki. 3 (sing only) mkono, athari there's someone's ~ in this pana mkono wa mtu. 4 (sing only) at first ~ moja kwa moja I received the news from him at first ~ nilipata habari toka kwake moja kwa moja. at second ~ kwa kupitia njia nyingine I received the news about him at second ~ nilipashwa habari zake kwa kupitia mtu mwingine. 5 (sing only) ustadi, weledi he's a good ~ at something yu stadi wa kufanya kitu. get one's ~ in jizoeza (tena). keep one's ~ in dumisha umahiri (wa kufanya mambo). 6 mtendaji mzoefu; (labourer) kibarua, mfanyakazi; (nautical) baharia. all ~s watu wote, kila mtu. 7 mshiriki. have a ~ in something -wamo (katika jambo fulani). 8 (watch, clock etc) mshale, akrabu. 9 upande left ~ mkono wa kushoto right ~ mkono wa kuume (wa kulia). on every/either ~; on all ~s toka/kila upande, pande zote. on the one ~ kwa upande mmoja. on the other ~ kwa upande mwingine. 10 (sing only) mwandiko he writes a legible ~ mwandiko wake unasomeka. 11 (formal) sahihi given under my ~ and seal idhinishwa kwa sahihi na muhuri wangu. 12 (cards) karata (alizoshika mchezaji). have a good/bad/poor ~ -wa na karata nzuri/mbaya. play a good/bad ~ cheza (karata) vizuri/vibaya. play into somebody's ~s fanya jambo litakalo mnufaisha mtu mwingine; mchezaji (karata); mchezo mmoja (wa karata). take a ~ at something shiriki; cheza karata. 13 kipimo kama inchi nne; nusu shubiri. 14 (colloq) makofi. give somebody a good ~ pigia makofi. 15 (compounds) handbag n begi, mkoba. hand-barrow n mkokoteni unaosukumwa. handbill n tangazo (linalotolewa kwa mkono). ~ book n kiongozi, kijitabu cha maelekezo. ~ brake n breki ya mkono. handclap n (pigo la) makofi. handcuff n pingu. vt tia pingu. handful n -chache; kiasi kidogo; konzi; ukufi only a ~ of people attended the meeting watu wachache tu walihudhuria mkutano; kiasi cha kuweza kujaza kitengele; (colloq) tukutu, sumbufu. hand-grenade n kombora la mkono. ~-hold n kishikizi; kitu cha kushika wakati wa kupanda. ~-luggage n mizigo ya mkononi. ~ made adj -a mkono; -liotengenezwa kwa mkono. ~ maid n mjakazi, mtumishi wa kike. ~-me -down n mtumba. kitu ambacho kimeshatumika. hand-picked adj -liochaguliwa kwa makini. handrail n papi za ngazi. handsaw n msumeno (wa mpini mmoja). handshake n kupeana mikono. handstand n kusimama kwa mikono. handwork n kazi ya mkono. handwriting n mwandiko, mkono. handy adj 1 fundi, -epesi. ~ly adv kwa kazi (hasa za mikono). ~y man n mtu mwepesi wa kazi (hasa za mikono): wepesi kufanya kazi yoyote. 2 (of things, place) -a kuchukulika;(useful) -a kufaa kutumiwa kwa urahisi come in ~y faa wakati mwingine. 3 karibu, tayari,-siokuwa mbali. handily adv handiness n.hand
2 vt 1 pa; leta; saidia kwa mikono please ~ me that pencil tafadhali niletee kalamu hiyo. 2 ~ down (to) rithisha the house was ~ed down to his son mtoto wake alirithi nyumba yake. 3 ~ something on to somebody pitisha please ~ this book on to Mary tafadhali nipitishie kitabu hiki kwa Maria. 4 ~ out (to somebody) (colloq) toa sadaka. hand-out n taarifa iliyotayarishwa na mkuu na kutolewa (agh. kwa waandishi wa habari); (of school) kitini; sadaka kwa maskini. 5 ~ over (to somebody) peleka mtu kwa polisi n.k.. ~ something over (to somebody) kabidhi. 6 ~ it to somebody (colloq) msifu mtu; -pa (mtu) haki yake.