grow

vi,vt 1 kua; mea, ota the child is ~ing well mtoto anakua vizuri maize ~ well in Iringa mahindi yanaota vizuri huko Iringa. ~ out of -wa kubwa kuliko/kua; zidi. 2 (increase) zidi, ongezeka. ~ on/upon zidi kupendeza she ~s on you anazidi kukupendeza the book grows on me kitabu kinaniteka, kinazidi kunipendeza; acha kufanya (kwa uzee) I' ve ~n out playing football nimeacha kucheza mpira; tokana na his troubles ~ out of his laziness matatizo yake yanatokana na uvivu wake. ~ up komaa, pevuka, -wa -zima what do you want to do when you ~ up? unataka kufanya nini utapokuwa mtu mzima?; kua friendship grew up between the two students urafiki ulikua kati ya wanafunzi hawa wawili. ~ing pains n pl maumivu ya viungo; (fig) matatizo ya mwanzoni mwa shughuli fulani ~n up n mtu mzima. 3 -wa ~ older konga, chakaa ~ smaller pungua ~ taller refuka. ~ dark -wa giza. 4 (agrc.) panda, lima, otesha he ~s three crops a year anapanda mara tatu kwa mwaka. 5 fuga, acha kitu kikue ~ a beard fuga ndevu, acha ndevu zikue. 6 ~ to be/like etc zoea I grew to like cheese when I lived in Germany nilipokuwa Ujerumani nilianza kuzoea jibini. grower n 1. mwoteshaji 2. mmea (unaokua kwa njia fulani) a fast/slow ~er mmea unaokua upesi/polepole. growth n 1 kuzidi; kukua; ukuaji. 2 ongezeko. ~th rate n kima cha ongezeko. 3 (vegetatition) ulimaji, uotaji this year's ~th of maize has been good uotaji wa mahindi mwaka huu ulikuwa mzuri. 4 maendeleo; kuenea eneo. 5 maotea. 6 (med) kushika ugonjwa k.m. kansa, donda ndugu.