get

vi,vt 1 (obtain, receive) pata ~ a present pata zawadi. ~ an illness pata ugonjwa. 2 -wa ~ wet rowa ~ lost (sl) ambaa! potea! ondoka! 3 fanya, sababisha ~ the food ready andaa chakula. ~ something done kamilisha, maliza kufanya. 4 anza; anzisha ~ going anza when the women ~ talking wanawake wanapoanza kuongea. 5 pata (kujua, kusikia, n.k.) when you ~ to know her you will like her utakapomfahamu vizuri utampenda. 6 shawishi, leta you'll never ~ him to understand huwezi kumwelewesha I can't ~ him to talk nashindwa kumshawishi aongee. 7 pewa adhabu ~ six months pewa kifungo cha miezi sita. ~ told off (colloq) semwa, karipiwa. 8 (colloq) elewa, pata I didn't ~ the joke sikuuelewa mchapo wenyewe I don't ~ you sikuelewi/pati. 9 (esp. in perfect tenses) tatanisha, pata I have got you there! Nimekupatia! 10 -wa na, miliki we have got a big house tuna nyumba kubwa. 11 have got to paswa, lazima I have got to finish this job lazima nimalize kazi hii. 12 weza, fanikiwa. 13 (non idiomatic intransitive uses with adverbial particles and preps) enda. ~ across vuka. ~ back rudi. ~ home fika nyumbani. ~ off toka. ~ a move on fanya haraka where can it have got to? iko wapi/imepotelea wapi? ~somewhere piga hatua. ~ nowhere/not ~ anywhere -tofika popote. ~ there (colloq) fanikiwa. 14 (non idiomatic transitive uses) peleka. patisha: I'll ~ you home before midnight nitakurudisha kabla ya saa sita usiku ~ your clothes on vaa I'll ~ you to the station early nitakupeleka/fikisha stesheni mapema. 15 (idiomatic uses with adverbial particles and preps) ~ about (of somebody who has been ill) tembeatembea, pata nafuu; (of news, rumour, story) enea; (of a person infml) safiri, zunguka. ~ above oneself jivunia, jiona. ~ something across (to somebody) (colloq) elewesha. ~ ahead (of somebody) pita (mtu); fanikiwa zaidi. ~ along weza; endelea; ondoka. ~ along with elewana na/patana na. ~ along with you! (colloq imper) ondoka; acha! usiniambie! ~ around see ~ round. ~ at somebody/something fikia; pata. ~-table adj -enye kufikika; -enye kupatikana. ~ at somebody (bribe) honga, -pa rushwa; (taunt) chokoza, kera. ~ at something gundua, pata ~ at the truth gundua/pata ukweli. be ~ting at (colloq) maanisha. ~ away toroka. ~ -away n kutoroka make one's ~ away toroka. ~ away with something fanikiwa bila kugunduliwa (katika jambo ovu) you'll never ~ away with it watakugundua. ~ back rudia kwenye madaraka (baada ya kuyapoteza). ~ back at somebody/~ one's own back (on somebody) lipa kisasi. ~ by pita/kubalika, weza, ishi. ~ down (of children) ondoka mezani (baada ya kula); shuka, teremka; shusha. ~ somebody down (colloq) sononesha; fadhaisha. ~ something down (swallow) meza; (write) andika. ~ down to something anza kufanya kitu kwa makini. ~ home (to) somebody eleweka wazi. ~ in fika; (to a car etc) panda; (of election) chaguliwa. ~ somebody in ita mtu (fundi, daktari n.k.) nyumbani (ili kutoa huduma). ~ something in kusanya; jaliza, weka akiba. ~ into (of clothes) vaa; ingia katika hali fulani ~ into trouble ingia matatani. ~ a girl into trouble (colloq) tia msichana mimba. ~ into bad company shirikiana na waovu; jifunza, zoea. ~ into one's head that elewa kuwa. ~ off anza. ~ off lightly/cheaply -topata adhabu kali. tell somebody to ~ off/where he ~s off (colloq) -pa mtu ukweli wake. ~ somebody/-something off tuma, peleka (barua n.k.). ~ off (bus etc) shuka, telemka. ~ somebody off okoa (kwenye adhabu). ~ somebody off to sleep laza. ~ something off ondoa; vua. ~ something off (by heart) kariri. ~ off with somebody (colloq) fanya mapenzi na. ~ off with something pata (adhabu ndogo) he got off with a fine alipata faini tu. ~ on endelea, songa mbele; (of time) pita. ~ on something panda. ~ on one's feet simama; (fig) pata nguvu mpya; fufuka, inuka. be ~ting on for (of time age) karibia. ~ on to somebody wasiliana na (colloq) tambua/gundua (ujanja, hila n.k.). ~ on (with somebody) elewana/patana na. ~ on (with something) endelea na. ~ on with it! fanya haraka! ~ out (of secret etc) julikana, fichuka. ~ something out (of words) sema; (of produce) toa; chapisha; tawanya; (of meeting etc) ondoka. ~ out of (doing) something kwepa; (fig) acha polepole. ~ something out of somebody pata jambo kutoka kwa mtu. ~ over somebody (colloq) sahau. ~ over something (of ilness etc) pata ahueni/nafuu; (overcome) shinda. ~ something over (with) maliza, fikia mwisho wa (kitu kibaya au chenye matatizo). ~ something over (to somebody) elewesha I can't ~ over it nashindwa kuamini. ~ round somebody shawishi mtu. ~ round something epa; zunguka. ~ round to doing something (pata muda wa kushughulikia jambo (baada ya mengine yenye maana kushughulikiwa). ~ through (to) fikia, fika, wasiliana na. ~ through (something) pita, faulu, shinda ~ through an examination faulu mtihani. ~ through (with) something maliza, fikia mwisho. ~ through to somebody that elewesha mtu/pasha mtu habari kuwa. ~ somebody through (something) saidia mtu kushinda/kufaulu. ~ something through hakikisha jambo linatekelezwa; (of proposal, bill in parliament etc) pitisha kuwa sheria; pitisha. ~ to fikia hali fulani. ~ together kutana (kwa dhifa, majadiliano n.k.). ~ together n kukutana; mkusanyiko (kwa ajili ya tafrija, mkutano n.k.). ~ it/something together (colloq) panga, ratibu/simamia jambo. ~ oneself together (colloq) weza kujizuia; jitawala. ~ people/things together kusanya. ~ up inuka; (from bed) amka; (mount) panda; (of wind, sea) anza kuchafuka/ kucharuka. ~ somebody/something up inua; amsha, andaa vizuri (kitabu n.k.). ~ up n mtindo/mpango wa kitabu/jarida/mavazi (hasa usio wa kawaida). ~ something up tayarisha, panga. ~ up to something fikia; shughulika/fanya lisilo la kawaida. ~ somebody with child (arch) tia mimba.