generate

vt fanyiza; leta; zalisha ~ electricity zalisha umeme. generator n jenereta. generation n 1 kizazi three generations vizazi vitatu (baba na wanawe na mjukuu). 2 kufanyiza, kuzalisha. 3 kizazi: kipindi cha wastani cha umri wa mtu wa kuoa na kuwa na watoto. 4 rika, watu waliozaliwa wakati mmoja, wa rika moja. generative adj -zazi generative organs viungo vya uzazi generative grammar sarufi fafanuzi/zalishi.