from

(prep) 1 (from a place, starting point) toka, kutoka he is ~ Tarime ametoka Tarime he is ~ home ametoka nyumbani where are you ~ umetoka wapi? 2 (starting a period of time) in the past tangu ~ childhood tangu utotoni ~ that day tangu siku ile ~ the beginning to the end tangu mwanzo hadi mwisho; (in the future) kuanzia ~ tomorrow kuanzia kesho. 3 (showing giver, sender etc) kutoka kwa a letter ~ my mother barua kutoka kwa mama yangu. 4 (separation, removal, prevention, escape) toka released ~ prison achiliwa kutoka gerezani refrain ~ laughing jizuia kucheka a shelter ~the rain kinga ya mvua. 5 (showing lower limit) kuanzia mangoes sell ~ shs 10/= embe zinauzwa kuanzia shilingi kumi. 6 (source taken from) -tokana na; kutoka kwa ideas drawn ~ Shaaban Robert mawazo yanayotokana na Shaaban Robert. 7 (material used in process) the bridge is made ~ steel daraja limetengenezwa kwa chuma (change) the price has risen ~ 20/= to 30/= bei imepanda kutoka sh 20/= hadi 30/=. 8 (distinction or difference) distinguish the good ~ the bad pambanua wema na ubaya (reason, cause, motive) kwa sababu ya what does it stem ~? sababu yake nini? ~ fatigue kutokana na uchovu. 9 (judging by) kwa kuangalia, kutokana na ~ her appearance you would think she was young kwa kuangalia umbo lake ungedhani ni kijana. 10 (with adv & prep phrases) ~ above/below toka juu/chini. ~ afar toka mbali. ~ over there toka kule.