free

adj 1 (of a person) huru; -ungwana; -siofungwa. freeman n muungwana. ~ born n, adj mtu huru. 2 (of a state, its citizens, and institutions) huru, -nayojitawala. 3 -siozuiwa; huria, -lioachwa huru. allow somebody/give somebody/ have a ~ hand -pa mtu/ ruhusu mtu/-wa na uhuru wa kufanya jambo bila kushauriana na mwingine/ wengine. ~ agent n mtendaji huria (awezaye kutenda jambo bila kizuizi). F~ church n Kanisa Huria; Kanisa lisilo chini ya udhibiti wa dola/serikali. ~ enterprise n uchumi huria. ~-and-easy adj bila taadhima. ~ fall n kuanguka/kujirusha toka kwenye ndege bila mwavuli (mpaka unapohitajiwa). ~ fight n mapigano ambayo yeyote aliyepo aweza kujiunga; mapigano yasiyo na kanuni. free-for-all ugomvi/majadiliano huria (ambayo yeyote anaweza kutoa maoni bila kuzuiwa). ~ hand adj (of drawings) -liochorwa kwa mkono tu (bila kutumia vifaa kama rula, bikari); -a kukakata. ~ handed adj karimu; si mkono wa birika. ~ hold n (leg) umilikaji ardhi bila masharti. ~ holder n mmilikaji ardhi asiyekuwa na masharti. ~house n (GB) kilabu cha pombe za aina zote. ~ labour n wafanyakazi wasio wanachama wa vyama vya wafanyakazi. ~ lance n (in middle ages) mamluki; mwandishi/ mtengenezaji filamu huria (anayetoa huduma zake popote). vi fanya kazi ya uandishi huria. ~ liver n mwanisi: mtu ajiingizaye kwenye raha (hasa ya chakula na vinywaji) bila kizuizi. ~ living n adj maisha ya anasa. ~ love n (old use) uhusiano wa mapenzi bila kuoana; mapenzi huria. ~ kick n (football) mpira wa adhabu. ~ port n bandari huria (ambayo wafanyibiashara wote wanaweza kuitumia bila vizuizi vya kodi n.k.). ~ range adj (of poultry) -a kienyeji; -siofungiwa ndani. ~ free speech n uhuru wa kusema. ~ spoken adj bila kuficha mawazo; -liosemwa kwa bahati. ~ standing adj -siotegemezwa popote. ~ stone n jiwe mchanga. ~ style n (swimming) mashindano yasiyo na mkambi maalumu. ~ thinker n mtu asiyefuata mafundisho ya dini ya asili bali atumiaye mantiki. ~ thinking adj bila kufuata mapokeo ya vitabu vya dini. ~ thought n fikra zisizofuata mapokeo ya dini. free-trade n biashara huria (bila vikwazo vya kodi, ushuru). ~-translation n tafsiri isiyo ya neno kwa neno. ~-verse n shairi guni. ~-way n (US) baraste. ~-wheel vi enda kwa baiskeli bila kupiga pedali, (fig) tenda/ishi kwa kujiamulia. ~-will n hiari (ya moyo), utashi. ~-will adj -a hiari. 4 ~ from bila. ~ of nje ya; bila. 5 bure, pasipo malipo admission ~ kiingilio bure ~ of income tax pasipo malipo ya kodi ya mapato get for ~ pata kitu bure. ~ list n orodha ya watu wa kuingia bure; orodha ya vitu vinavyoweza kuingia bila kulipiwa ushuru wa forodha; ~ on board n (abbr fob) (comm) huduma hadi bandarini. ~ pass n ruhusa ya kusafiri bure/bila kulipa nauli. ~-loader n (sl) doezi. 6 (of place or time) bila shughuli; isiyotumiwa (of persons) bila kazi. have one's hands ~ -wa bila shughuli; -wa katika hali ya kuweza kujiamulia mambo. 7 -ja/toa kwa wingi a ~ flow of water mtiririko wa maji mengi. 8 bila aibu/kizuizi. make ~ with tumia kitu bila aibu (kama chako). 9 make somebody ~ of -pa mtu haki ya uwanachama wa kikundi, uraia n.k. freeman n mtu aliyepewa haki ya uraia wa jiji. vt ~ (from/of) 1 weka huru, komboa; okoa. 2 ondosha; komesha, batilisha ~ a country of cholera komesha kipindupindu katika nchi. 3 ondolea kizuizi/shida/matata. ~d man n mtumwa aliyeachiwa huru. freedom n 1 uhuru the ~dom of the seas (international law) haki ya meli kusafiri baharini bila kuingiliwa na manowari give a friend the ~dom of one's house -pa rafiki ruhusa ya kutumia nyumba kama yake. 2 hiari, chaguo. 3 give/receive the ~dom of a town/city -pa mtu/pokea haki zote za uraia wa mji/jiji. ~domfighter n mpigania uhuru.