for

for

1 (prep) 1 (indicating destination or progress towards) set out ~ the beach elekea pwani passengers ~ Mombasa abiria waendao Mombasa. 2 (indicating intention) built ~ rough roads -lioundwa kwa barabara mbovu. 3 (indicating ultimate possession) make some coffee ~ the guests tayarisha kahawa kwa ajili ya wageni. be ~ it (colloq) weza kuadhibiwa au kupata shida, pata you are ~ it now utaipata sasa. 4 (indicating preparation for) be ready ~ the long drought jiandae kwa ukame wa muda mrefu. 5 (indicating purpose) read ~ fun soma kwa kujifurahisha. what ~ kwa sababu/ kazi gani. 6 (introducing complement) they were taken ~ crooks walidhaniwa wahuni. ~ certain kwa uhakika/yakini. 7 (with an object of hope, wish, search, inquiry etc) hope ~ the best omba Mungu. 8 (indicating endowment) an aptitude ~ mathematics kipaji/ kipawa cha hisabati. 9 (indicating liking) has a taste ~ wine anapenda mvinyo. 10 (indicating suitability) a man ~ the job mtu anayefaa kazi. 11 (after adj) too little ~ the day's wage kidogo mno kwa ujira wa siku. 12 kwa kuzingatia it is quite an achievement ~ a foreigner ni mafanikio makubwa kwa mgeni. ~ all that licha ya yote hayo. 13 (representing) mwakilishi, kwa niaba ya; badala ya, kwa/badala ya. stand ~ wakilisha. 14 (in defence or support of) she was ~ mult- partism aliunga mkono/alitetea vyama vingi. 15 (with regard to) ~ my part kwa upande wangu I am hard up ~money kuhusu fedha nimeishiwa kabisa. 16 kwa sababu ya blame ~ the delay laumu kwa (sababu ya) kuchelewa. 17 (after a comparative) my shoes are the worse ~ wear viatu vyangu vimezidi (kwa) kuchakaa. 18 licha ya; dhidi ya ~ all you say, I still enjoy his company bado nafurahia usuhuba wake licha ya yote usemayo. 19 kwa kiasi cha reserve two seats ~ $ 50 weka/shika viti viwili vya (kiasi cha) $ 50. 20 (in exchange for) plant two trees ~ every tree you cut down panda miti miwili kwa kila mti unaoukata. 21 (in contrast with) ~ one enemy she had a hundred friends kwa kila adui mmoja alikuwa na marafiki mia moja. 22 (duration) I shall be away ~ three weeks nitakuwa sipo/ nitaondoka kwa majuma matatu. 23 (distance) we walked ~ twenty kilometers without meeting a soul tulitembea kwa kilomita ishirini bila kukutana na mtu. 24 (as part of the subject) ~ a man to chair a women's association is impossible kwa mwanaume kuwa mwenyekiti wa chama cha wanawake ni muhali.

for

2 conj kwa kuwa; kwani, kwa maana, maana I asked her to join us ~ she was all alone nilimtaka aungane nasi kwani alikuwa mpweke. forage n 1 chakula cha farasi (punda, ng'ombe). 2 kutafuta chakula. (mil) ~-cap n kofia ya kazi ya askari. vt ~ (for) tafuta chakula, tafuta (kitu chochote); nyang'anya. ~ for oneself jitegemea. ~r n mtafutaji chakula.