foot

n 1 mguu, kanyagio, wayo. on ~ (kwenda) kwa miguu, kwa kutembea; (fig) -lioanzishwa tayari the project is on ~ mradi umeshaanza (na sasa unaendelea). be on one's feet -wa wima; simama, inuka (ili kusema jambo fulani) the Minister was on his feet at once to answer the charge Waziri alisimama mara moja kujibu shitaka; (fig) -wa na afya njema baada ya kuugua. fall on one's feet (colloq) -wa na bahati, bahatika. have feet of clay -wa mnyonge au mwoga. have one ~ in the grave karibia kufa (k.m. kutokana na uzee), chungulia kaburi. keep one's feet -toanguka (k.m. wakati unatembea kwenye utelezi. put one's ~ down (colloq) kataa; pinga; shikilia msimamo. put one's ~ in it (colloq) sema au fanya kosa au upuuzi; boronga. put one's feet up (colloq), pumzika huku miguu imenyooshwa, miguu juu. put one's best ~ forward tekeleza kazi yako haraka iwezekanavyo. set something/ somebody on its/his ~ wezesha mtu/kitu kijitegemee. set something on ~ anzisha kitu/jambo. sweep somebody off his ~ tia mtu ari/jazba, hamasisha sana. under ~ chini, ardhini. 2 hatua, mwendo swift of ~ mwendo wa haraka, mwendo mwepesi. 3 sehemu ya chini (ya kitu); tako at the ~ of a hill chini ya mlima. 4 sehemu ya mwisho ya mguuni mwa kitanda au kaburi. 5 (measure) futi. 6 kipimo cha mkazo katika mashairi. 7 (mil. old use) askari wa miguu. 8 (compounds) ~-and mouth disease n shuna, ugonjwa wa midomo na miguu. ~-ball n soka, kandanda. ~ bath n beseni la kunawia miguu. ~-board n kibao cha mwinamo anachokanyaga dereva. ~-bridge n daraja la waendao kwa miguu. ~-fall n sauti ya hatua. ~-fault n (sport (tennis) kosa la hatua (la kuruka msitari wakati wa kupiga mpira mara ya kwanza). ~-hills n vilima vidogo chini ya mlima mkubwa au safu za milima mikubwa. ~-hold n (in climbing) kidato; (fig) mahali pa usalama. ~-lights n taa za chini za jukwaa. the ~-lights (fig) kazi ya uigizaji. ~ loose; ~ loose and fancy free adj huru bila dhima. ~-man n mtumishi wa kiume, mkaribishaji wageni; mtumishi anayekuwa mezani wakati wa chakula. foot-mark n see ~-print; ~-note n rejeo/tanbihi chini ya ukurasa. ~-path n njia ya miguu. ~-plate n (of a train) kijukwaa cha kusimamia dereva na mchochea moto. foot-pound n kipimo cha kazi (cha kunyanyua ratili moja futi moja). ~-print n wayo. ~-race n mashindano ya mbio. ~-rule n rula ya mti au metali (urefu wa inchi 12). foot-slog vi (colloq) enda mbali kwa hatua kubwa na kishindo. ~-slogger n (colloq) mwendaji wa miguu, mtu anayekwenda mwendo mrefu kwa miguu. foot-sore adj -enye jeraha la miguu kutokana na kutembea. ~-step n sauti ya hatua; wayo. follow in one's father's ~ step fuata vitendo vya baba; fuata nyanyo. ~-stool n kibao cha kuwekea mguu. ~-sure adj -siotetereka; -siochukua hatua potovu; imara. ~-wear n (tradesman term for) viatu. ~-work n namna ya kutembeza miguu kwenye dansi au mchezo wa ngumi. vt,vi 1 fuma mguu wa soksi. 2 ~ it (colloq) nenda kwa miguu, tembea. ~ the bill (colloq) lipa (gharama). footed adj (in compounds) -enye miguu kama ilivyoonyeshwa. sure -~ed adj -siotetereka, imara. footing n (sing only) 1 usimamaji; mahali pa kusimamia he lost his ~ ing aliteleza; alikunguwaa. 2 nafasi (katika jamii kikundi n.k.). be on a friendly ~ing with (your neighbours) -wa na uhusiano mzuri na majirani zako. 3 hali on a peace/war ~ing katika hali ya amani/vita. footage n urefu unaopimwa kwa futi (hasa filamu). footer n 1 (colloq) soka, kandanda. 2 (compounds) a six-~en n mtu mwenye urefu wa futi sita.