fly

fly

1 n nzi. a ~ in the ointment dosari ndogo inayochafua sherehe/furaha. there are no flies on him (fig sl) mjanja, yu mwerevu. (compounds) fly-away adj (of clothes) -a kupwaya; (of persons) badhirifu; -liopoteza fikra. fly-blow n yai la nzi. fly-blown adj (of meat) -lioanza kuoza (kwa sababu ya mayai ya nzi ndani yake); (fig) chafu; bovu. fly-boat n mashua ieleayo. flybook n kijaruba cha kuwekea chambo (nzi) cha kuvulia samaki.fly-by-night n mtu atembeaye usiku; mtu asiye mwaminifu. fly-catcher n mtego wa nzi; shore kishungi, tiva. fly-fish vi vua samaki kwa nzi bandia. ~fishing n kuvua samaki kwa nzi bandia. ~ing-leaf n ukurasa mtupu usiopigwa chapa (mwanzoni au mwishoni mwa kitabu). ~-over n (US = over pass) barabara, daraja n.k. ipitayo juu ya barabara nyingine. (GB) flypast n gwaride la Wanaanga. fly-wheel n gurudumu tegemeo. ~-paper n karatasi yenye kunata ya kunasia nzi. fly-sheet n waraka/sekula ya kurasa. ~-swatter; ~-whisk n mwengo, mgwisho. ~-trap n mtego wa kunasia nzi. ~-weight n (of boxing) uzito wa chini. ~er;flier adj 1 mnyama, gari n.k. liendalo kasi mno. 2 mfanyakazi ndani ya ndege hasa rubani. flying adj 1 -a kuruka. 2 -a muda mfupi; -a haraka, -a mbio sana. 3 -siyokazwa; -a kupwaya. 4 (compounds) ~ing -ant n kumbikumbi. ~ ing boat n ndege (eropleni) ya majini. ~ing -bomb n roketi yenye bomu la kupiga mbali. ~ing -club n chama cha watu wapendao mchezo wa kuruka (hewani). ~ing -colours n bendera za kupamba/kupepea (agh. wakati wa sherehe). ~ing -column n (mil) kikosi cha jeshi chenye uwezo wa kwenda haraka na kufanya mashambulizi chenyewe. ~ing -field n uwanja wa ndege. ~ing -fish n panzi la bahari: samaki wa nchi za tropiki awezaye kuruka. ~ing -fox n nundu. ~ing -jump n urukaji unaoanza kwa kukimbia. ~ing -saucer n kisahani kinachosemekana kilionekana kikipita angani. ~ing -squad n kikosi cha polisi cha kufukuza wahalifu chenye gari za kasi sana. ~ing -visit n ziara ya muda mfupi; kupitia.

fly

2 vi,vt 1 ruka, puruka. ~ high -wa na tamaa ya (kuendelea, kukuza hali n.k.). ~ up ruka angani. the bird has flown mtu anayetafutwa ametoroka. 2 endesha ndege (hewani n.k.); safiri; safirisha (kwa ndege) every day people ~ to Zanzibar from Dar es Salaam kila siku watu husafiri kwa ndege kwenda Zanzibar kutoka Dar es Salaam. 3 kimbia; kimbilia; enda mbio, pita upesi. ~ off toka (enda) ghafla. ~ open funguka (dirisha, mlango n.k.) ghafla. ~ at somebody rukia, shambulia. ~ in the face of pinga; kana; katalia hadharani/wazi; kuwa dhidi ya/kinyume kabisa cha mambo. ~ into a rage /passion/temper pandwa na hamaki, hasira. ~ to arms twaa silaha kwa ari. ~ to bits/~into pieces pasuka na kutawanyika vipande vipande. ~ to the rescue kimbilia kuokoa maisha. make the feathers/fur ~ sababisha fujo/ugomvi. make the money ~ fuja mali. send somebody ~ing piga/gonga mtu ili aanguke kifudifudi au kwa mgongo. send things ~ing vurumisha vitu pande zote. 4 rusha (tiara, kishada) hewani; pandisha bendera. 5 hajiri.

fly

3 n 1 (also colloq, pl. used with sing. meaning) lisani, mhalibori. 2 kipande cha turubali kwenye mlango wa hema au gari. 3 ncha ya bendera iliyo mbali na mlingoti.

fly

4 adj (sl) -erevu, janja; -siodanganyika.