fire
n 1 moto. lay a ~ koka moto. light/make a ~ washa moto. set on ~ choma moto, tia moto, unguza. make up a ~ chochea. catch ~ shika moto. between two ~s katikati ya hatari mbili. set on ~ choma moto. strike ~ from pekecha moto. he never set the Thames on ~ hatatia fora; hatafanya la ajabu. there is no smoke without ~ (prov) pafukapo moshi pana moto. play with ~ chezea moto/hatari. 2 (blaze) mwako; uteketezaji. ~ and sword mauaji na uteketezaji (vitani). ~ risks(s) visababisha moto. 3 (brightness) wangavu. 4 (excitement) juhudi, harara. 5 (energy) nguvu. 6 mshindo wa bunduki; kupiga bunduki. open/cease ~ anza/ simamisha mashambulio. under ~ shambuliwa. running ~ n mfululizo wa mashambulio; (fig) mfululizo wa maswali, shutuma n.k. 7 (comp. words). ~-alarm n king'ora (cha moto). ~ arm n silaha ya moto, bunduki, bastola, n.k. fire-ball n kimondo; (mil.) sehemu ya katikati ya bomu la atomi. firebird n ndege wa kimarekani mwenye rangi ya manjano na nyeusi. firebomb n bomu la moto. firebox n chumba cha fueli. firebrand n kijinga cha moto; (fig.) mchochezi wa mambo (katika jamii au kisiasa). firebreak n kinga ya moto sehemu iliyolimwa na kukatwa miti kusudi kuzuia moto usiingie katika msitu. firebrick n tofali lisiloathiriwa na moto. ~ brigade n zimamoto: kikosi maalum cha kuzima moto. firebug n (sl) mtu mwenye kuchoma nyumba kusudi. ~ clay n udongo usioshika moto, agh. hutumiwa kwa kutengenezea matofali ya kukinga moto. ~ control n udhibiti (wa) mapigo ya bunduki. ~ cracker n fataki. ~ damp n mitheni. ~ dog n see andiron. fire drill n mazoezi ya utaratibu unaotakikana kufuatwa kama kumetokea moto. ~eater n mshari. ~ engine n gari la zima -moto. ~escape n ngazi/njia ya kinga (ya) moto, ngazi za wazimamoto za kuokolea watu (wakati wa hatari ya moto). ~extinguisher n kizima moto: kifaa cha kuzimia moto. firefighter n mzimamoto (hasa moto wa misitu). firefly n kimemeta, kimulimuli. fireguard n kiunzi cha waya wa metali cha kuzuilia moto. ~hose n bomba la mpira la kuzimia moto. ~irons n vichocheo, koleo ya moto. firelight n mwangaza wa moto; kijinga; tita la kuni la kuwashia moto. fireman n mwangalizi wa moto katika tanuu au injini ya moto; mzimamoto. fireplace n mekoni; ukingo wa fito wa kuzuilia moto nyumbani; jiko. ~ plug n plagi, kiunganishio cha mpira wa zimamoto. firepower n uwezo wa kupiga silaha (unaopimwa kwa idadi na uzito wa milipuko kwa kila dakika). fireproof adj -sioungua, -sioshika moto. ~raising n uchomaji nyumba kwa makusudi. fireside n sebule ya kuotea moto sit at the ~ side (fig) tulia nyumbani; ishi maisha ya nyumbani. ~station n makazi ya zima moto na vifaa. firestone n jiwe lisoshika moto. ~walking n tambiko au sherehe ya kukanyaga mawe ya moto kwa miguu mitupu. ~ water n (colloq) pombe kali hasa kama vile wiski, jini n.k.. firewood n kuni. fire-work n fataki: chombo chenye baruti na kemikali kitumiwacho kwa kufanyia michezo. vt,vi 1 tia moto, choma moto, unguza, teketeza. 2 kaanga, choma, oka katika tanuu. ~ bricks choma matofali. 3 chochea kuni. 4 piga bunduki ~ a salute toa salamu ya heshima (kwa kupiga mzinga). ~ a shot piga bunduki. ~ at/into/on/ upon something/somebody piga risasi, fyatulia risasi. ~ away endelea kupiga risasi. firing line n mstari wa mbele wa mashambilizi. firing squad/party n kikosi cha wauaji/watoa salamu za rambirambi (jeshini) (colloq) anza mara moja. 5 fukuza kazini. 6 (kwa bunduki) lia. 7 lipuka; waka. ~ up (usu flare up) kasirika, hamaki, sisimua. ~ somebody with something sisimua, tia hamu, hamasisha.