find
find
1 n ugunduzi; kitu cha thamani kilichopatikana agh. kwa bahati.find
2 vt 1 ona, pata (baada ya kutafuta kitu kilichopotea). ~ one's voice/ tongue weza kuzungumza (baada ya kuwa kimya). 2 tambua, ng'amua ~ a solution to the problem ng'amua utatuzi wa tatizo. ~ one's feet anza kusimama na kutembea (k.m. mtoto); weza kufanya mambo bila kutegemea wengine. ~ oneself jitambua, jijua. 3 fika, fikia water always ~s its own level maji hufikia usawa wake. 4 gundua, kuta (kwa bahati); tambua. ~ somebody (out) gundua. ~ somebody out gundua mtu akifanya kosa. 5 ona, kuta, ng'amua do you ~ that hard work brings rewards? unaona kuwa bidii inalipa? take us as you ~ us tuchukulie kama tulivyo. 6 tafutia, toa; patia. ~ somebody oneself in patia/jipatia (kitu). all found patiwa kila kitu wanted a good cook, 6000 shillings a month and all found anatafutwa mpishi mzuri, mshahara shilingi 6000 na atapatiwa chakula na malazi bure. 7 (leg) hukumu, amua. ~ for amua kutoa ushindi kwa ~ for the defendant upande wa utetezi umeshinda. 8 ona how did you ~ the play? uliuonaje mchezo? 9 ~ out chunguza, tafiti, tafuta ~ out the price of coffee tafuta bei ya kahawa. finder n 1 mtu apataye/aonaye kitu kilichopotea. 2 (of camera) kitafuta kilengeo. finding n (usu pl) 1 matokeo. 2 uamuzi wa mahakama.