figure

n 1 (number) tarakimu (hasa kutoka 0 mpaka 9). double ~s n makumi: tarakimu kuanzia 10 hadi 99. single ~s n mamoja/epesi. 2 (pl) hesabu quick at ~s -elekevu wa kuhesabu. 3 (appearance) umbo. have a fine ~ -wa na umbo zuri. cut a fine/poor/sorry ~ onyesha sura nzuri/mbaya/ya masikitiko. 4 mchoro (k.m. wa mtu, mnyama, ndege n.k.), sanamu. ~ head n sanamu ya kuchonga (ya kichwa na kifua tu au umbo zima) inayotumiwa kama pambo juu ya gubeti; (fig) mkubwa wa jina tu, mtu mwenye cheo kikubwa lakini kisicho na madaraka hasa/ya haja. 5 bei buy something at a low ~ nunua kitu kwa bei ndogo what is your ~? kiasi gani? wauzaje? 6 mtu, hasa tabia yake dominating ~ mtu mashuhuri sana. 7 ~ of speech n tamathali ya usemi. 8 mchoro, kielelezo, chati n.k.. vt,vi 1 fikiria/waza moyoni; onyesha. 2 ~ (in) onekana; jitokeza, wa mashuhuri he ~s in Kiswahili yu mashuhuri katika Kiswahili. 3 ~ something out elewa, piga hesabu. ~ somebody out elewa mtu I can't ~ that man out simwelewi mtu huyu. 4 ~ (on) (US) kisia, kadiria, dhani, tegemea I ~ him (to be) honest nadhani yu mwaminifu. 5 (represent) -wa mfano wa. figured adj -liotiwa nakshi. figuration n ufanyizaji wa umbo; umbo; uumbaji wa taswira. figurative adj -a kitamathali, kistiari, -a methali. figuratively adv. figurine n sanamu ndogo.