field

n 1 mbuga ya malisho, shamba a ~ of wheat shamba la ngano. 2 (usu in compounds) uwanja a landing ~ (for aircraft) uwanja wa ndege. ~ events n pl mashindano ya kuruka/kutupa (si ya kukimbia). ~ glasses n bainokula/darubini. ~sports n michezo ya nje, kuwinda, n.k. 3 (usu in compounds) eneo la machimbo, mgodi gold ~ mgodi wa dhahabu. 4 uwanja wa kitaaluma this is in my ~ hili lipo katika uwanja wangu (wa kitaaluma). ~ work n utafiti ufanywao nje ya maabara/maktaba, utafiti/kazi ya uwandani. 5 eneo (la matumizi n.k.) magnetic ~ eneo la sumaku. 6 (mil) uwanja wa mapambano battle ~ uwanja wa vita. ~ day n siku ya mazoezi ya kijeshi; (fig) siku maalum. have a ~ day (fig) fanya sherehe, -wa na ushindi. ~ hospital n hospitali ya muda vitani. F~ Marshal n Jemadari Mkuu. ~ gun n mzinga. 7 (sports and athletics) washindani/washiriki wote; wasasi wote. vt,vi 1 (cricket and baseball) -wa tayari kudaka au kuzuia (mpira) she ~ed the ball well aliudaka mpira vema. 2 (of football teams) ingiza; panga, chezesha timu uwanjani. fielder n ; ~ sman n (cricket etc) mdaka/ mzuia mpira. 3 (colloq) jibu he ~ed that question well alijibu vizuri swali hilo.