feel

n (sing only) 1 the ~ n hisia za kugusa (mfano ugumu, ulaini, uororo n.k.). 2 the ~ n msisimko unaotokana na kuguswa au kupapaswa. 3 kugusa. 4 get the ~ of anza kuzoea. vt,vi 1 hisi, jua kwa kugusa/kushika n.k. ~ the pulse hisi/pima mapigo ya moyo. ~ one's way tembea kwa uangalifu (kama katika giza au kipofu afanyavyo), papasa; tahadhari katika kutenda mambo fulani. 2 ~ (about) (for) papasa papasa, tomasa, sunza he felt about in the dark for his bed alisunza ili aone kitanda chake. 3 (through contact) sikia I can ~ a thorn in my shoe nasikia mwiba ndani ya kiatu changu. 4 (not through contact) ona. (to) ~ the weight of something fahamu umuhimu wa jambo fulani I ~ it my duty to natambua ni wajibu wangu the chairman felt the force of his argument mwenyekiti aliona uzito wa hoja yake. ~ somebody out jaribu kujua maoni ya mtu kwa uangalifu. 5 jisikia, jiona, ona I ~ ill najisikia mgonjwa. to ~ quite oneself kujiona barabara ~ cold/ happy ona baridi/ furaha. 6 -wa na uwezo wa kuhisi a corpse does not ~ maiti hana uwezo wa kuhisi. 7 ~ for/with one; ~ pity for somebody onea huruma, hurumia. 8 ~ as if/ though hisi/jihisi kana kwamba he felt as if he was flying alijiona kana kwamba alikuwa anapaa. 9 onekana, onekana kama it ~s like wood inaonekana kama ubao it ~s soft inaonekana ororo. 10 ~ like (of persons) jisikia, taka, penda, pendelea we shall go together if you ~ like it tutakwenda wote ukipenda. ~ equal to jihisi sawa na; (colloq) ~ up to -wa na nguvu/uwezo wa. 11 patwa na, sumbuliwa na she ~s the loss of her father msiba wa baba yake unamhuzunisha he does not ~ the cold at all baridi haimsumbui. 12 fikiria kwamba, waza kuwa, onelea the committee felt the project to be feasible kamati imefikiria kwamba mradi unawezekana kutekelezwa. 13 furahia, changamkia, elewa vizuri. ~ er n (of insects, animals) 1 papasi. 2 (test) hoja itolewayo ili kupima mawazo ya watu wengine. put out ~s/a ~ pima mawazo ya wengine kwa kuwapa maswali maalum. feeling n 1 uwezo wa kuhisi the ~ing in his legs is weak uwezo wa kuhisi katika miguu yake ni dhaifu.2 hisia a ~ing of hunger hisia ya njaa. a ~ing of joy hisia ya furaha; (of an opinion) (usu sing) wazo la wote. 3 (pl) hisia za mtu hurt a man's ~ings udhi mtu, tia uchungu wa moyo. 4 huruma; uelewano he does not show much ~ ing for the sufferings of others hana huruma na wenziwe, haonei huruma wenzake. good ~ing n urafiki, uelewano. ill/bad ~ing n chuki, uhasama. 5 chuki; hasira his failure aroused strong ~ings in teachers kufeli kwake kumeibua chuki kubwa miongoni mwa walimu wake. 6 mapenzi he has much ~ing for (art, beauty etc.) ana mapenzi makubwa ya (sanaa, uzuri n.k.) adj -enye huruma; -ema; -enye kuonyesha hisia zake. feelingly adv.