fact

n 1 tendo, jambo ambalo limetendeka au limefanywa. accessary before the ~ (leg) mtu aliyemsaidia mhalifu kabla ya tendo kufanyika. accessary after the ~ (leg) mtu aliyemsaidia mhalifu baada ya tendo. 2 ukweli, jambo la hakika. a ~ of life ukweli usioepukika. the ~s of life (colloq, euphem) maelezo kuhusu jinsi watu wanavyozaliana (kama wanavyosimuliwa watoto). ~ finding adj -enye kutafuta/ kuchunguza ukweli. in ~; in point of ~; as a matter of ~ kwa kweli. factual adj -enye ukweli. factum n (leg) kanuni, taarifa ya kweli.