face
n 1 uso, wajihi fall on one's ~ anguka kifudifudi. bring two parties ~ to ~ kutanisha pande mbili ili zikabiliane. come ~ to ~ with somebody kutana uso kwa uso. look somebody in the ~ kazia mtu macho. be unable to look somebody in the ~ shindwa kumtazama mtu kwa sababu ya aibu au woga. set one's ~ against somebody pinga sana. show one's ~ tokea, onekana, jitokeza ili kuonekana. in (the) ~ of kabiliwa na, licha ya I could do nothing in the ~ of these problems sikuweza kufanya lolote nilipokabiliwa na matatizo haya. fly in the ~ of pinga waziwazi. in one's~ ; in the ~ usoni, pajini; pasipo kujaribu kuficha death stared at him in the ~ alijikuta kwenye mauti. to one's ~ bayana (bila kuficha au kuogopa) tell him so to his ~ mweleze bayana. 2 (compounds) ~ ache n kipanda uso. ~ card n karata ya sura ya mzungu. ~ cloth n taulo ndogo ya kunawia uso. ~ cream n krimu ya uso. ~ lift(ing) n operesheni ya ngozi ya uso (kufanya uonekane laini/wa kijana). ~ powder n poda ya uso. 3 (expression/look) sura. keep a straight ~ -toonyesha hisia. make/ pull ~s geuza/finya uso. put on/wear a long ~ onekana mwenye kufikiri sana au kuhuzunika. 4 (various senses) have the ~ (to do something) thubutu. lose ~ adhirika. put a good/bold/brave ~ on fanya ionekane kuwa nzuri, -wa na ujasiri wa kukabili jambo. put a new ~ on badili sura ili ionekane tofauti. save (one's) ~ jiepusha na aibu. ~ saver n tendo la kuepusha aibu . ~ saving n,adj. on the ~ of it inavyoonekana. 5 sura, sehemu ya mbele north ~ of the mountain upande wa kaskazini wa mlima a diamond has many ~s almasi ina sura nyingi. ~ value n thamani liyoandikwa. (fig) at ~ value bila kuangalia kwa undani; (fig) jinsi kitu au mtu anavyoonekana kijuujuu. 6 ukubwa na mtindo wa sura ya kalibu ya kuchapa. faceless adj (fig) -sojulikana/tambulika. vt 1 elekea, tazama, kabili the house ~s the bank nyumba inatazamana na benki. About/Left/Right ~ (US mil. commands) = (GB) About/ Left/Right turn) nyuma/kushoto/ kulia geuka. 2 kabili (kwa kujiamini). ~ it out kabili kishujaa. ~ the music kabili matatizo/hatari n.k. (bila kuogopa). ~ up to kubali hali ilivyo. let's ~ it (colloq) lazima tukiri. 3 tambua kuwepo kwa. 4 kabili the problem that ~s us tatizo ambalo linatukabili. 5 ~ (with) funika kwa tabaka la kitu kingine n (GB dated, colloq) tatizo kubwa linalomkabili mtu ghafla au pasipo kutegemea. facial adj -a uso. facial massage n kukanda na kupodoa uso. facing n 1 kibandiko. 2 mkono, mpako (wa rangi au kitu tofauti) k.m. kwenye ukuta.