express

express

1 adj 1 halisi; dhahiri, wazi. ~ condition n sharti dhahiri an ~ command amri dhahiri. 2 (speedy) -a kwenda mbio sana, isiosimama mara kwa mara, -a haraka an ~ letter barua ya haraka an ~ train treni ya moja kwa moja; treni kasi. ~ way n (US) barabara pana (kwa ajili ya magari yaendeshwayo kwa kasi). n 1 treni kasi. 2 (US) kampuni ya kusafirisha mizigo kwa haraka na usalama. 3 huduma za haraka (zitolewazo na posta, reli na barabara za kusafirisha mizigo, n.k.). expressly adv 1 kabisa, kwa dhati, kwa hakika you are ~ly forbidden to go huruhusiwi kabisa kwenda. 2 hasa, kwa madhumuni ya the function was ~ly for children only tamasha ilikuwa hasa kwa watoto tu.

express

2 vt 1 peleka kwa njia ya haraka barua/mzigo; eleza; dhihirisha, onyesha; simulia. ~ oneself jieleza n.k. 2 ~ (from/out of) (formal) kama, kamua. expression n 1 (facial) sura she had an ~ion of sorrow alikuwa na sura ya huzuni. 2 (words) neno, usemi, msemo. beyond/past ~ion isiyoelezeka (to) give ~ion to something dhihirisha/ eleza jambo fulani. find ~ion in jitokeza katika, jidhihirisha kwa. 3 (feeling) onyesha hisia she sang with ~ion aliimba kwa kuonyesha hisia. 4 (Maths) uonyesho. 5 (pl) cognate ~ions n misemo ya mshabaha, misemo inayoshabihiana, misemo inayofanana. 6 kusema freedom of ~ ion uhuru wa kusema/kutoa mawazo. expressionless adj. expressive adj. ~ive (of) -enye maana, -enye kuelezea, -enye kuonyesha hisia. expressiveness n. expressionism n (of painting, part, etc) fasihi halisia-nafsi. expressionist n.