exercise

n 1 (use) matumizi;kutumia the ~ of the imagination matumizi ya ubunifu the ~of his duty shows his zeal utekelezaji wa wajibu wake unaonyesha bidii aliyonayo ~ of patience subira. 2 (practice) mazoezi he does ~s every morning anafanya mazoezi kila siku asubuhi. 3 jaribio, shindano, zoezi the pupils were given an ~ by their teacher wanafunzi walipewa zoezi na mwalimu wao. ~ book n daftari (la mazoezi). 4 (usu pl) mazoezi ya kijeshi, drili. 5 (US pl) sherehe graduation ~ mahafali. vt,vi 1 tumia ~ authority tumia madaraka. ~ patience fanya subira. 2 fanya mazoezi; zoeza; jizoeza you don't ~ enough hufanyi mazoezi ya kutosha. 3 (usu passive) sumbua, hangaisha (moyo) this problem is exercising our minds tatizo hilo linasumbua akili zetu. exercitation n (arch) 1 mazoezi. 2 onyesho la umahiri.