escape

n 1 kutoroka, utorokaji. 2 kuokoka, kuponyoka; njia/chombo cha kuokolea/kutolea kitu/mtu he had a narrow ~ aliponea chupuchupu. ~ velocity n kasi mwelekeo ya kuponyokea: kasi inayohitajika kukiwezesha chombo fulani (hasa cha anga) kujitoa kwenye eneo la nguvu za mvutano fulani; (of gas, smoke, etc) mvujo, kuvuja; chombo cha kutolea mvuke, gasi, n.k. an ~ pipe bomba la kutolea moshi, mvuke n.k. an ~ valve vali ya kutolea hewa, kupumulia n.k. 3 kimbilio: kitu kinachobadilisha/sahaulisha mawazo kwa muda, mfano muziki, michezo, kileo, n.k. escapee n mtoro, mfungwa aliyetoroka. escapism n ukwepaji (wa matatizo). escapist n mkwepaji, mtu mwenye tabia ya kukwepa/ kukimbia (mambo). vt,vi 1 ~ (from) toroka, kimbia, toka the prisoner has ~d mfungwa ametoroka gas ~s from an open pipe gasi hutokea kwenye bomba lililo wazi. 2 okoka, nusurika, epa he ~d from injury amenusurika. 3 -toangaliwa, - totambuliwa; sahauliwa, pitiwa this issue ~d my notice suala hili limenipitia.