equal

adj 1 sawa, sawasawa, -a kulingana twice three is ~ to six mbili mara tatu ni/sawa na sita all things being ~ mambo yote yakiwa sawa. on ~ terms kwa usawa (to) get ~ with somebody kulingana na fulani. 2 ~ to something/to doing something -enye uwezo/ujasiri be ~ to the ocasion weza, mudu, -toshindwa. are you ~ to it? waiweza? n 1 (in age) hirimu, marika. live as ~s ishi kama marika kwa usawa. 2 (in condition, quality) mwenzi she has no ~ hana kifani. vt -wa sawa na, lingana na, landana. equality n. equalitarian n see egalitarian. equalize vt sawazisha. equalization n ulinganifu, usawazishaji. equalizer n kisawazishaji. equally adv.