end

n 1 mwisho, kikomo the ~ of the road mwisho wa barabara. begin/start at the wrong ~ anza vibaya. get hold of the wrong ~ of the stick elewa vibaya. keep one's ~ up (GB) endelea/wa na uso mkunjufu hata katika matatizo. at a loose ~ bila chochote cha kufanya. on ~ wima place the box on its ~ simamisha kasha wima; mfululizo, bila kukoma four hours on ~ saa nne bila kukoma. ~ on ncha zinapokutana. ~ to ~ kutana/ kutanisha ncha kwa ncha. go (in) off the deep ~ chukua bila kujizuia; shindwa kujizuia. make (both) ~s meet ishi kulingana na kipato chako. (reach) the ~ of the line/road (fig) fikia mahali ambapo huwezi tena kuendelea. 2 kipande kilichobakia a cigarette ~ kipande cha sigara kilichobakia. ~ papers n kurasa tupu za mwisho wa kitabu. endpoint n hatua ya mwisho ya jambo. 3 mwisho, kikomo, hatimaye the ~ of the month mwisho wa mwezi the ~ of the story mwisho wa hadithi. (be) at the ~; at the ~ (of) mwisho the fighting was at an ~ mapigano yalifikia kikomo. come to an ~ isha the conference came to an ~mkutano uliisha. come to a bad ~ isha vibaya; adhirika if you don't stop racketeering you will come to a bad ~ usipoacha ulanguzi mwishowe utaadhirika/utafungwa jela. draw to an ~ karibia mwisho. make an ~ of something; put an ~ to something komesha. in the ~ hatimaye. no ~ of (colloq) mno, sana he thinks no ~ of himself anajiona sana. without ~ pasipo kufikia mwisho, bila mwisho. 4 kifo she is nearing her ~ anakaribia kufa. 5 kusudi, madhumuni, lengo gain one's ~ pata kitu mtu alichokusudia to no ~ bila mafanikio. the ~ justifies the means (prov) kusudi zuri huhalalisha njia ya kulifikia, bora kufika. vt,vi maliza, isha the game ~s here mchezo unaishia hapa ~ your argument malizeni ubishi wenu. ~ in something -wa matokeo ya; ishia the plan ~ed in failure mpango haukufaulu. ~ off maliza he ~ed off teaching at 2.00 pm alimaliza kufundisha saa nane mchana. ~ up ishia, maliza, hitimisha if you go on stealing you will ~ up in jail ukiendelea kuiba utaishia kifungoni. ending n mwisho, kikomo. ~ less adj -siokuwa na mwisho, -enye kuendelea ~less chain mnyororo usiokuwa na mwisho (ambao mwisho wake umeunganishwa). endmost adj mwisho kabisa. ~ways; ~wise adv pembe hadi pembe, mwishoni, kwa (kutanguliza) mwisho.