earth

n 1 the ~ dunia; ulimwengu; ardhi. come down/back to ~ ondoka ruuyani/ndotoni. 2 uso wa dunia (to) drop to ~ tua ardhini; (dry land as opposed to sea) nchi kavu. move heavens and ~ (to do something) fanya juu chini kupata jambo. how/why/where/who, etc. on earth vipi tena/mbona/wapi sasa/nani tena. 3 (soil) udongo. ~ closet n choo, lindi. ~ nut n karanga. ~ work n boma la udongo. ~ worm n nyungunyungu. 4 (animal's hole or lair) pango, shimo (la mnyama). run/go to earth (of a fox) kimbilia shimoni. run something/somebody to ~ (fig) saka, gundua baada ya kutafuta sana. 5 (elect) waya au njia ya kugusia kukamilisha mzunguko wa umeme. vt 1 ~up funika kwa udongo, fukia. 2 (elect) tia waya wa umeme ardhini. 3 (of fox) jificha pangoni. earthborn adj -liozuka ardhini; -liozaliwa duniani, -a binadamu. earthbound adj (fig) -enye mwanzo wa kilimwengu, -enye kuelekea duniani; -sioweza kuacha dunia; -sio bunifu. earthen adj -a udongo, -liofinyangwa. earthenware n vyombo (vitu) vya udongo. earthly adj 1 -a dunia hii. 2 (colloq) -a kuwezekana; -enye kufikirika. no ~ly use (colloq) haifai hata kidogo there is no ~ly chance (sl) hakuna uwezekano. earthquake n zilizala: tetemeko la ardhi. ~ shine n mwako wa dunia: mwangaza unaotoka duniani na kuonekana kwenye sehemu ya kiza ya mwezi. earthy adj 1 -a udongo. 2 (fig) fidhuli.