drive
vt 1 swaga. ~ somebody into the corner (fig) weka mtu katika hali ngumu, bana sana. 2 endesha (motokaa, garimoshi n.k.). driving licence n liseni ya kuendeshea gari. driving school n shule ya udereva. driving test n mtihani wa udereva. driving lessons n mafunzo ya udereva. 3 chukua/peleka kwa gari ~ a friend to town mchukue rafiki mjini (kwa gari). 4 enda/tembea kwa gari. ~ in n (and attrib.) mgahawa, sinema n.k. ambako watu huingia na magari yao. 5 (usu passive) endesha. driving belt n ukanda wa kuendeshea. 6 (of wind, water) peleka/tupa/sukuma. 7 (of rain, ship) enda upesi au kwa nguvu/ kwa kasi. 8 ~ in; ~into pigilia, kongomea. 9 piga kwa nguvu. ~ home (fig) elewesha barabara. let ~ at piga, rushia kombora, lenga. 10 sababisha; fanya (kitu kitokee), lazimisha. 11 sulubisha, fanya/ fanyisha kazi sana. ~ away at (one's work) fanyia kazi sana. 12 fukua; toboa (kwa nguvu) (shimo, tundu). 13 endesha shughuli (agh. biashara). ~ a hard bargain -wa mkali kwenye biashara, -wa mgumu. 14 ~ at -wa na maana ya; maanisha; kusudia. 15 ahirisha. 16~ off fukuza, rudisha nyuma n 1 (in US also ~ way) njia ya binafsi ya kwenda nyumbani. 2 matembezi kwenye gari ya binafsi to take for a~ kutembeza ndani ya gari (ya binafsi). 3 nguvu ya kupiga/kurusha mpira; mpigo. 4 bidii, nguvu, wepesi; uwezo wa kuendesha mambo, msukumo. 5 kampeni. 6 mashindano. 7 (mech) chombo cha kuendeshea. right hand ~ n kuendeshea kulia. four wheel ~ n endesha kwa magurudumu manne. driver n 1 dereva be a good/bad ~r kuwa dereva hodari/asiyefaa. 2 msimamizi (wa gari, farasi, watumwa). in the ~r's seat kwenye uongozi; (mech) kiendesha mitambo. 4 (golf) rungu ya kupigia mpira mbali; kingoe. driving adj -enye nguvu/uwezo.