drain

vt 1 ~ away/off toa maji kwa mifereji/bomba. 2 kausha. ~ing board n kichanja cha kukaushia vyombo. 3 (drink) -nywa yote. 4 ~ (away/off); ~ (of) (fig) fifisha, dhoofisha, nyonya ~ somebody of his strength etc. chosha mtu. 5 nyonya usaha, unyevu (kwa bomba). 6 nywa/maliza kunywa (agh. ndani ya glasi). 7 ~ the cup of pitia (hasa matukio/maisha mabaya). n 1 mfereji, mfumbi, bomba la kutoa maji. throw money down the ~ ponda mali, tumia pesa vibaya. go down the ~ potea bure, teketea, haribika. 2 jambo linalofifilisha/nyonya. brain ~ n uhamaji wa wasomi/mabingwa toka nchi moja hadi nyingine (wakitafuta maslahi). 3 kinywaji kidogo, tone. drainage n 1 mtiririsho. 2 (sewers) mfereji, bomba la maji machafu. ~age system n mfumo wa kuchukua maji machafu. ~age-area/~basin n eneo ambalo maji ya mto hutokea. ~age-tube n (med) neli ya usaha.