domestic

adj 1 -a nyumbani, -a jamaa a ~ person mtu anayependa kukaa nyumbani, mkaa nyumbani ~ science sayansi kimu, maarifa ya nyumbani. 2 -a nchini, -a ndani, -a kienyeji. ~ flights n safari za ndege za ndani. ~ news n habari za nchini. 3 (of animals) -liofugwa na binadamu; -enye kukaa na binadamu. a ~ animal n mnyama anayefugwa n mtumishi wa nyumbani. domestically adv. domesticate vt (chiefly in pp) 1 idilisha; zoeza kazi za nyumbani she's not at all ~ated hapendi/hawezi kazi za nyumbani. 2 (of animals) fuga. domestication n. domesticity n 1 (kupenda) maisha ya nyumbani, maisha ya familia. 2 (pl) mambo ya nyumbani.