dog

n 1 mbwa; mbwa dume. 2 (in phrases) every ~ has his day kila mtu ana siku yake, iko siku. give a ~ bad name (and hang him) paka mtu matope/haribu jina la mtu (na watu wataendelea kumfikiria vibaya). help a lame ~ over a stile saidia mtu wakati wa dhiki/matatizo. let sleeping ~s lie acha mambo kama yalivyo, usimwamshe aliyelala, ukimwamsha utalala wewe. love me love my ~ ukimpenda baniani upende winda wake. he doesn't stand/have (even) a ~'s chance hana uwezo wowote (wa kushinda, kushiriki). go to the ~s potoka, haribika; haribikiwa, kwisha. throw/give to the ~s tupa (kama takataka), sukumiza. lead a ~s life ishi maisha ya taabu. lead somebody a ~'s life sumbua/ghasi mtu kila wakati treat somebody like a ~ tendea vibaya, dhalilisha a ~ in the manger mtu mwenye inda (anayewazuia wengine wasifaidi kitu fulani ambacho hakimsaidii yeye). be the under ~ -wa mtu wa kushindwa tu. be top ~ (colloq) -wa kiongozi, -wa mwenyewe. die a ~'s death/die like a ~ -fa kifo cha aibu/dhiki. dressed like a ~'s dinner (colloq) amevalia maridadi sana/kufuata mitindo mipya kabisa. look like a~'s breakfast/ dinner onekana shaghala- baghala. a case of ~ eat ~ hali ya unyang'au. you can't teach an old ~ new tricks (prov) si rahisi kumbadilisha mzee. 3 (colloq) jamaa. a sly ~ n mtu mjanja. 4 a hot ~ n mkate wenye soseji. 5 (in compounds). ~ biscuit n biskuti za mbwa. ~'s body n mtu wa chini (afanyaye kazi za ovyo). ~collar n mkanda wa mbwa; (colloq) kola ya padre. ~days n siku za jua kali. dog-eared adj ( of a book) -enye visikio, -enye vikunjo. dogfight n mapigano baina ya ndege za kivita. doghouse n kibanda cha mbwa. (sl) be in a ~ house aibika. dog-paddle n mtindo wa kuogelea kama mbwa. be dog-tired -wa taabani kwa uchovu/kuchoka sana. dog-watch n (naut) zamu ya saa mbili katika meli dogvane n (naut) kibendera. ~ eat ~ adj katili -a unyang'au. doglike adj a kama mbwa. doggy/ doggie n (child's word for) mbwa vt fuata karibu sana, andama. ~ somebody's footsteps fuata mtu kila aendapo. dogged adj (obstinate) -kaidi, shupavu, -gumu. 2 (firm) kakamavu, -siokata tamaa, thabiti.