distance

n 1 umbali; masafa, kitalifa part of the ~ sehemu ya umbali (fulani) a good ~off mbali kidogo na hapo a short ~ from karibu na. at a ~ kwa mbali within calling ~ karibu vya kutosha kusikika/kuitika, kitambo kidogo. in the ~ huko mbali. keep somebody at a ~ fanya mtu asikuzoee. keep one's ~ (fig) kaa mbali, jitenga usizoeleke. some ~ mbali kiasi within walking ~ karibu tu. long ~ adj (of races, journeys) -a masafa marefu, mbio ndefu, safari ndefu; (of telephone calls) simu kutoka/kwenda mbali. middle ~ adj (of races) mbio za umbali wa kati. 2 (space of time) muda, kitambo vt ~(from) weka/kaa mbali na, pita mbali kabisa, acha nyuma. distant adj 1 distant (from) -a mbali have a distant recollection kukumbuka kwa mbali a distant relative ndugu wa mbali. 2 (of degree of similarity) -siofanana sana, -a kufanana kidogo sana. 3 (cold, reserved) -siozoeleka, baridi, si -kunjufu we are on distant terms hatukuzoeana sana. distantly adv.