democracy

n 1 demokrasia: mfumo wa serikali unaoshirikisha wananchi kupitia wabunge (waliochaguliwa). 2 nchi yenye kuhimiza na kuruhusu haki za uraia kama uhuru wa kusema, kuabudu, kutoa maoni na kushiriki, kusisitiza utawala wa sheria, utawala wa walio wengi, pamoja na kuheshimu haki za wachache. 3 jamii ambamo watu wote ni sawa na hakuna hisia za kitabaka. democratic adj 1 -a demokrasi, -enye kuunga mkono demokrasi; -a kidemokrasi. democrat n 1 mwanademokrasia; mpenda demokrasia. Democrat n (US) mwanachama wa Chama cha Democrat. democratize vt fanya iwe -a kidemokrasi; fanya -a demokrasi. democratization n.