damp

vt,vi (also dampen). 1 fifiza kazi/nguvu ya kitu; punguza mbembeo polepole hadi kusimama kabisa. 2 tilia gesi yenye sumu; palia kooni. 3 fanya kuwa na unyevunyevu ~ somebody's spirits punguza ari ya mtu ~ down a fire punguza mwako wa moto (kwa kutia majivu); (fig) punguza (furaha, raha, n.k.). 4 (of voice or musical instrument) punguza sauti. 5 ~ off (of plants) oza kwa unyevu mwingi n 1 unyevu, umajimaji. 2 harufu mbaya ya hewa au gesi yenye sumu (hasa katika mgodi wa makaamawe). 3 hali ya kukatisha tamaa adj 1 pwetepwete, -a majimaji, chepechepe kidogo; -bichi kidogo. ~ clothes n nguo zenye unyevunyevu. 2 -enye ari ndogo; -enye hali ya kupombogea/kutia majonzi/masikitiko. cast a ~ over (fig) tia mashaka/masikitiko/ wasiwasi; punguza matumaini. 3 (also fire ~) -a gesi ya sumu/hatari. dampness n unyevunyevu, umajimaji, upwetepwete