damn

vt 1 laani, apiza. 2 (of God) hukumu kwenda motoni, tia/takia adhabu ya milele. 3 sema kuwa kitu fulani ni hafifu; shutumu; puuza, toa thamani a book ~ed by the critics kitabu chapwa (kwa maoni ya wahakiki) ~ with faint praise sifu kidogo (kiasi cha kuonyesha kuwa hupendi). 4 (as interj to express strong emotion) I'll be ~ed if I accept your order sikubali kamwe/ng'oo! maagizo/amri zako ~ you mshenzi we! ~ his impudence ufidhuli wake ulaaniwe n 1 matusi. 2 I don't give/care a ~ hainiumi sikio wala ndewe; sijali kabisa. not worth a ~ bila thamani. damnable adj (also damned) 1 -a kuchukiza mno; (colloq) baya sana sana he spoke ~ well aliongea vizuri sana you 'll get ~ all hupati kitu. 2 -a kustahili laana, -enye kulaaniwa milele; maluuni. damnation n 1 kulaani/kulaaniwa, ulaanifu. 2 laana: adhabu ya kutengwa na Mungu. eternal ~ation n laana ya milele.