cry
vi,vt 1 toa sauti, guta, paza sauti; piga yowe. 2 lalama, lalamika. ~ for the moon omba miujiza. 3 lia, toa machozi. ~ one's eyes/heart out lia sana. ~ oneself to sleep lia mpaka kupatwa usingizi. give a child something to ~ for/about adhibu mtoto kwa kulia pasi sababu. 4 tangaza. 5 ~ at lilia, pigia kelele. ~ down dharau, shusha heshima, punguza thamani. ~ off jitoa (katika jambo uliloahidi au kupatana juu yake). n 1 kilio, mlio, ukelele, ukemi. give a ~ piga kelele. in full ~ (of dogs) bweka wote pamoja; (of peoples) (fig) shambulia (mtu) much ~ and little wool (prov) mwenye kelele hana neno. within ~ (of) hapa hapa, kando. 2 (of sorrow) yowe, unyende. 3 (of happiness) kigelegele, hoihoi. 4 (of complaint) lalamo. 5 kugutia. (fig) a far ~ mbali sana; tofauti sana. 6 kilio have a good ~ lia sana ili kupata tulizo have one ~ out acha alie mpaka atulie. crying n, adj kubwa sana. ~ing need n haja kubwa sana. ~ing-baby n mlialia.