compose

vt,vi 1 fanyiza, tengeneza be ~d of -wa na sehemu (nyingi); tengenezwa kwa; umbwa kwa it is ~d of rock -metengenezwa kwa jiwe. 2 tunga, buni, andika (wimbo, shairi, mawazo, hotuba). 3 (printing) panga herufi za chapa ili kuunda maneno au sentensi. 4 tuliza. ~ oneself jituliza, -wa makini. composed adj tulivu. composedly adv. composer n mtungaji. composing frame n fremu ya kupanga herufi. composing machine n mashine ya kupanga herufi. composing stick n chombo cha kuwekea herufi. composition n 1 utungo, insha, kitu. 2 kazi ya sanaa k.v. kitabu, maandiko, nyimbo n.k. 3 utungaji/usanii wa kitu. 4 (agreements) mapatano. composition of creditors n mapatano ya wawia. 5 (mixture) mchanganyiko. 6 (ingredients) vijenzi, sehemu mbalimbali, asili za kitu. 7 kupanga herufi za chapa. 8 (Maths; Physics) kivungo. composite adj -enye sehemu (vitu, tabia) zaidi ya moja, -liofanywa na sehemu nyingine au na vitu mbalimbali. compositor n mpanga herufi za chapa. composure n utulivu, makini.