common

adj 1 -a pamoja,-a wote. a ~ land n ardhi ya wote, ardhi ya umma. ~ consent n makubaliano ya pamoja/wote. ~ knowledge n habari inayojulikana na wote. ~ ground n (fig) hoja inayokubaliwa na wote katika majadiliano. ~ room n (in schools, college) chumba cha mapumziko. 2 -a kawaida. ~ soldier n askari wa kawaida, kuruta. ~ sense n maarifa ya kawaida. ~ practice n jambo la kawaida (kutendwa). 3 (Math) -a shirika ~ factor/multiple kigawo/kigawe shirika. (GB) ~ Law n sheria zisizoandikwa. ~-law wife n kimada. ~ market n soko la ushirikiano/ pamoja. 4 ~ noun (gram) n nomino ya jumla. 5 (colloq) (of persons, their behaviour and possessions) hafifu, -baya. ~ manners n tabia mbaya. commonly adv, n 1 eneo la ardhi lisilo na mwenyewe, ardhi ya jumuiya yote. 2 in ~ kwa ajili ya wote, kwa wote. in ~ with pamoja na; sawa na out of the ~ si -a kawaida. commoner n mwanachi wa kawaida. commons n (pl) (arch) 1 umma. 2 the House of C~ n (sometimes the Commons) Bunge la Uingereza lililochaguliwa na wananchi). 3 short ~s n uchache/upungufu wa chakula be on short ~s -topata chakula cha kutosha. commonalty n watu wa kawaida, makabwela. commonwealth n 1 dola; jumuiya ya madola. 2 The C~wealth n (also ~wealth of Nations) Jumuiya ya Madola: jumuiya ya nchi huru zilizokuwa chini ya utawala wa Kiingereza.