come

vi 1 ~ (to/from) (with) ja, wasili, fika ~ and see me njoo tuonane ~ this way pita huku. 2 ~ (into/ onto/in/on etc) ingia. ~ into the room ingia/karibu chumbani. 3 ~to something fikia the number of his children ~s to thirty idadi ya watoto wake inafikia thalathini. ~ to little/nothing tofanikiwa, -wa kazi bure she never came to much hakufanikiwa. ~ to this/ that maanisha, wa na maana ya, -wa hivyo (ilivyo) if it ~s to that kama mambo ndiyo hayo. (with fixed phrases) ~ to an agreement afikiana. ~ to blows (with) anza kupigana. ~ to a decision amua. ~ come to an end isha; malizika. ~ to fruition iva, komaa, zaa matunda. ~ to a halt/standstill simama. ~ to light julikana, tangazwa. ~ to one's notice/attention tambuliwa fahamika. ~ to one's senses/oneself zinduka pata fahamu; jirudi. ~ to terms (with somebody) fanya suluhu, kubaliana, afikiana. 4 (tokea) (anza) kuwa. ~ into flower tokea/anza kuwa ua; chanua. ~ into bud chipua. ~into contact kutana, gusa,wasiliana. ~ into focus jitokeza, jiengua. ~ into money/ a fortune/legacy etc rithi/ pata/pesa. ~into operation anza kufanyakazi. ~ into one's own stahiki, pata heshima/sifa. ~ into power twaa madaraka.~ into sight/ view tokeza, onekana. 5 ~ to somebody (from somebody) achiwa, rithi (shwa). 6 ~ to somebody tukia, tokea, -ja nothing will ~to you hutadhurika. 7 elewa/tambua/ona hatimaye. ~ to realize -ja kung'amua. 8 how ~ (that) vipi, imekuwaje. 9 ja, jia; tokea; wa (mahala) her decision came as a surprise uamuzi wake ulitushangaza. 10 -wa, tokea kuwa, -ja kuwa. be as clever/stupid as they ~ kuwa hodari/ mpumbavu sana. 11 (colloq) jifanya, jitia don't ~ the bully usijitie ungambi/ubabe/ umwamba. 12 to ~ baadaye the life to ~ maisha ya baadaye. 13 (colloq uses) ifikapo, ijayo she will be 15 ~ December atakuwa na miaka 15 ifikapo Desemba. 14 (colloq) (of sex) mwaga/tema/kojoa (with adverbials and preps) 1 ~ about fanyika, tukia, jiri. 2 ~ across kuta, kutana na; ona kwa bahati; tokea (kwa) I ~across John in the market nilikutana na John sokoni. 3 ~ after somebody fuatia, fukuzia, fuata kwa kukimbilia. 4 ~ again rudi. please ~ again karibu tena. 5 ~ against kuta, gongana; shambulia. 6 ~ along fanya haraka, jitahidi, endelea, fika ~ along now you know the answer jitahidi, unalijua jibu. 7 ~ alongside egeka, egemea. 8 ~ apart vunjika, katika, pasuka. 9 ~ at somebody/something fikia, pata, shambulia. 10 ~ away (from) achia, ondoka. 11 ~ back rudi, kumbuka his name came back to me nilikumbuka jina lake. ~ back at jibu, lipiza (kisasi). 12~ before somebody/something sikilizwa na, shughulikiwa na; tanguliwa na. ~ back n kurudi (tena); majibu; fidia his case will ~ before Judge Nyalali kesi yake itasikilizwa na Jaji Nyalali. 13 ~ between (interfere) ingilia kati; zuia it is not good to ~ between a man and his wife haifai kuingilia kati ya mume na mke. 14 ~ by pita; jia; pata kitu (kwa juhudi/bahati) ~ by my house pita nyumbani kwangu. 15 ~ down (collapse) anguka, poromoka; (of rain, snow etc) nyesha, -nya; (of prices) shuka, teremka; (be reduced) pungua. ~ down a peg shuka cheo. ~ down in the world angamia, shuka cheo. ~s /boils down to ~ ishia; maanisha; (of tradition) pokewa, rithishwa. ~ down upon kemea, adhibu, wia mkali. ~ down on the side of somebody unga mkono. ~ down to earth amini kama ilivyo, acha ndoto, tambua hali ilivyo. 16 ~ forth jitokeza, tokea mbele. 17 ~ forward karibia; jitokeza, jongea karibu, patikana. 18 ~ from zaliwa, chimbuka, tokea. 19 ~ in (of the tide) jaa (become seasonable) anza (kupendwa) when do mangoes ~ in maembe yanapatikana lini? (fashionable) how does this style ~ in mtindo huu unapendelewaje/ unapokelewaje? ~ in handy/ useful faa, -wa na manufaa. ~ in for, pata, vuta you'll ~ in for a scolding utakaripiwa she's ~ in for a large amount of money amerithi fedha nyingi. ~ in on shiriki, jiunga. 20 ~ near jongea, karibia he came near to failing alikaribia kushindwa. 21 ~ of -wa -a nasaba; tokana na; tokea she ~s of a given family -wa -a ukoo/ nasaba fulani what came of your conversation mazungumzo yenu yalikuwa na matokeo gani? 22 ~ off toka, tukia, fanyika; fanikiwa. ~ (something) dondoka; kimbia, okoka, banduka. ~ off a winner/loser shinda/ shindwa. ~ off victorious /badly pata ushindi/ hasara (colloq) ~ off it! acha! 23 ~ on fuata you go first I'll ~ on later tangulia nitakufuata baadaye; endelea his child is coming on fine mtoto wake anaendelea vizuri; kuta, vumbua, gundua. ~ on! njoo! endelea! (kwa mchezaji) anza kucheza ~ on let's have game njoo tucheze. 24 ~out tokea wazi, tangaa/bainika his book has ~ out kitabu chake kimechapishwa the whole affair has ~ out jambo lote limejulikana ~ out with a remark sema ghafula the workers will ~out again wafanyakazi watagoma tena. ~out first -wa wa kwanza ~ out in a rash pata vipele ~ out at so much afiki jumla (of stains etc.) these ink stains won't ~ out madoa haya hayatoki. ~out against/ for pinga/unga mkono. 25 ~ over (from a distance) fika; (change) geuka, enda upande mwingine, badili mawazo what has ~ over you limekutokea jambo gani ~ over funny/dizzy/faint jisikia vibaya, taka kuzimia. 26 ~ round zunguka; (visit) zuru, tembelea; (recover) pata fahamu ~ round to somebody's way of thinking badili mawazo. 27 ~ short of pungukiwa na; -wa na upungufu wa. 28 ~ through (recover from illness) pata nafuu, pona; pita your posting has just ~ through ajira yako imepitishwa. 29 ~ to pata fahamu ~ to one's senses pata fahamu baada ya kuzimia; husu when it ~s to politics inapohusu siasa; (colloq) jitambua. ~ to grief patwa na ajali (matata n.k.). ~ to a head iva. ~ to pass fanyika, -wa, tukia, jiri. 30 ~ under something -wa chini ya. 31 ~ up (grow) mea, ota, kua; fikia; (appear) tokea, zuka, onekana ~ up against somebody pambana, gongana, kutana your work has not ~ up to expectations kazi yako hairidhishi. ~up with fikia 32. ~ upon somebody shambulia ghafla.