clear

adj 1 -eupe, -angavu. 2 dhahiri, wazi make ~ eleza wazi; dhihirisha, funua. ~cut adj dhahiri kabisa ~ headed/sighted -enye kuelewa haraka a ~ case jambo la wazi, dhahiri. 3 bila kizuizi wala shida; bila shaka. it's ~ sailing hakuna taabu yoyote the coast is ~ hakuna hatari yoyote. 4 bila hitilafu, bila hatia/lawama, bila mgogoro. 5 kamili three ~ days siku tatu kamili ~ voice sauti wazi (isikikayo vizuri) ~ speaker msemaji asikikaye vizuri. ~ about/on -enye hakika. in the ~ -siotuhumiwa adv 1 kwa wazi, kwa dhahiri. 2 kabisa the prisoner got ~ away mfungwa alitoroka kabisa. 3 ~ (of) pasipo, bila, mbali na. vi,vt 1 safisha, takasa; safika, takata, ondolea (vizuizi, shida, mashaka, hatia). 2 epuka, jihadhari. keep ~ of something jitenga. 3 weka wazi. ~ the way! acha njia (iwe) wazi ~ the ground for negotations ondoa vikwazo ili kurahisisha mazungumzo. 4 (of liquids etc.) chuja. 5 fyeka ~ the bush fyeka magugu/gugu. 6 kiuka, pita juu ya au kando ya bila kugusa kitu. 7 pata faida ya we ~ ed shs 50,000 tumepata faida ya sh. 50,000.8 (tax etc.) lipa he ~ed his debts alilipa madeni yake. 9 ~ away ondoa ~ away the plates ondoa sahani; (of mist) tanzuka the clouds have ~ed away mawingu yametanzuka ~ (something) off ondoa, maliza (ote); uza rahisi; potelea mbali; (fig) penya, puruka. ~ out kumba; ondoka; ondoa. ~(something) up tengeneza, panga vizuri (of weather) takata; fumbua, tatua they ~ed their problems walitatua matatizo yao; safisha. clearly adv kwa dhahiri he is not ~ly intelligent ni dhahiri kwamba hana akili. 10 (pass over) pitisha (for cargo, ship) maliza taratibu za kuondoa (mizigo, meli) bandarini. 11 pata idhini (ya kuingia bandarini, kutua uwanjani). clearance n 1 kusafisha, kuondoa (vizuizi, shida n.k.). ~ance sale n seli ya kumaliza vitu. 2 ruhusa ~ance certificate hati ya ruhusa (ya kuondoa mizigo). 3 nafasi (iliyoachwa baina ya vitu viwili). 4 (mil) kibali cha kujiuzulu jeshini; kibali cha kusoma nyaraka za siri. clearing n 1 mahali peupe (pasipo miti katika mwitu); palipofyekwa, chenge. 2 tendo la kusafisha. clearing house n ofisi ya kubadilishia hundi za benki.