character

n 1 tabia; moyo; silika ya mtu, hulka. in/out of ~ ilio/isio kawaida (ya mtu fulani) he has a bad ~ana tabia mbaya. 2 sifa bainifu. 3 unyoofu, ukunjufu wa moyo takes ~ to speak the truth always inahitaji unyoofu kusema kweli daima. 4 mtu wa ajabu; wa tabia za kiajabu/kipekee that man is a real ~ mtu yule ni wa ajabu. 5 mhusika (katika riwaya, tamthiliya n.k.). 6 herufi in large ~s kwa herufi kubwa. 7 (arch) uthibitisho wa sifa zilizobainishwa. ~less (derog) bila sifa; -a kawaida. characteristic adj -a kawaida/tabia (ya mtu, kikundi) it is ~istic of him to ask for money ni kawaida yake kuomba hela n sifa bainifu what are the ~istics of a savannah plain? Ni nini sifa bainifu za ukanda wa savana? characterization n (lit) uchoraji, uumbaji wa mhusika (katika riwaya n.k.); ubainishaji wa tabia. characterize vt 1 eleza sifa (tabia, kawaida), ainisha. 2 -wa kawaida ya, -julikana kwa his work is characterized by sloppiness kazi yake huonyesha uzembe, the indigenous cow is ~ized by its hump ng'ombe wa kienyeji ajulikana kwa nundu yake.