catch

vt,vi 1 kamata, gwia, bamba ~a thief kamata/bamba/gwia mwizi. 2 shika, daka ~ the ball daka mpira ~a knife shika kisu. 3 (fig) pata, shikwa na ~ a cold pata mafua. ~fever shikwa na homa. 4 kuta, fuma I caught the boys stealing niliwakuta watoto wakiiba ~ somebody in the act of doing something gundua mtu kosa lake. 5 wahi. ~ a train wahi treni. ~ somebody fuma mtu akifanya jambo. 6 ~ (up) fikia aliye mbele you have to work hard to ~ up with the rest huna budi kufanya kazi sana uwafikie wenzako. 7 nasa, kwama the nail caught her dress msumari ulinasa nguo yake. 8 fahamu, tambua; sikia I ~ your meaning nafahamu maana yako. 9 ~ sight of ona kwa kitambo kidogo. 10 piga he caught me on the nose alinipiga pua. 11 pata you will ~ it utaipata; (of woman) (sl) pata mimba. 12 jaribu kushika. a drowning man ~es at straws mfa maji haachi kutapatapa. n 1 kudaka. 2 hila; mtego there's a ~ in it pana mtego. 3 vuo. 4 mwindo; pato la bahati. ~ one's breath ziba pumzi (kwa mshtuko). ~ fire shika moto. catcher n (basketball) mdakaji. catching adj 1 (esp. of disease) -a kuambukiza. 2 (attractive) -a kuvutia; -a kuwaka. ~ crop n mazao yanayokua kwa haraka sana yanayopandwa kati ya mimea mingine (k.m. maharage kati ya mahindi).