cast
vt 1 tupa, rusha. ~ a dice tupa dado. ~ an anchor tupa/tia nanga. ~ a vote piga kura. ~ing vote n kura makata. ~ something in somebody's teeth laumu. 2 kalibu, subu; mimina katika kalibu. 3 (of snake), jinyonyoa jichuna, jiambua. 4 ~ up jumlisha, kokotoa. 5 geuza, elekeza (macho). ~ about for angaza, tafutatafuta. ~ an eye over tupia jicho. 6 (theatre) pangia wahusika dhima katika mchezo. 7 (naut) legeza (kamba). 8 (printing) kadiria nafasi (itakayohitajiwa). 9 (knitting) ~ on fuma safu ya kwanza ya vitanzi. ~ a net tupa wavu. ~ a horoscope piga falaki, bao ~ a new light on a problem leta mtazamo/ mwanga mpya (juu ya jambo). ~ somebody aside achana na mtu, telekeza. ~ away (usually pass) acha (kutokana na kuvunjika kwa meli). ~ down sononesha ~ (in one's lot) with somebody jiunga pamoja na. ~ off anza safari. ~ off clothes tupa nguo. ~ offs n mitumba. ~ off legeza, fumua. ~ out toa, fukuza. ~ out devils fukuza pepo. ~ away n mtu aliyevunjikiwa na meli. adj -enye kuvunjikiwa na meli. n (throw) 1 mtupo, mrusho. 2. kalibu. ~ iron n kalibu ya chuma adj (fig) kaidi, bishi, gumu. 3 kitu kilichoumbwa katika kalibu. 4 (squint) kengeza kidogo. a ~ in the eye kuwa na kengeza kidogo. 5 wachezaji: seti ya wachezaji (k.m. katika filamu ya sinema) aina, sifa.