carry

vt,vi 1 beba, chukua, eleka she carried the child on her back alimweleka mtoto he is ~ing the load on his head ameubeba mzigo kichwani mwake. 2 peleka, pitisha the pipes ~ water to the town mabomba hupeleka maji mjini copper carries electricity shaba hupitisha umeme. 3 (conquer) shinda, faulu our team carried the day timu yetu ilishinda timu zote. ~ everything before one fanikiwa kila kitu, shinda kabisa. ~ one's point ungwa mkono. 4 himili these pillars ~ the weight nguzo hizi zinahimili uzito. 5 (be pregnant) she is ~ing a child yu mjamzito. 6 refusha, zidisha, endeleza ~ the wall to ten feet zidisha ukuta kufikia futi kumi. 7 (with phrases) ~ weight -wa na uzito your reasons ~ no weight sababu zako hazina uzito. 8 simama/ tembea they ~ themselves like soldiers wanatembea kama askari. 9 (of guns) enda mbali, fikia mahali/masafa. 10 (of disease) eneza. 11 ~ too far zidi; vuka mpaka. ~ about tembea na, enda na (kila mahali). ~ away beba. be carried away jisahau. ~ off nyakua, shinda; ua. ~ it off fanikiwa (katika hali ngumu) cholera carried off 10 people kipindupindu kiliua watu 10. ~ on endelea (licha ya matatizo); lalama. ~ (with) fanya mapenzi na. ~ings on vitendo vya kijinga/ajabu. ~ out maliza, tekeleza. ~ through kamilisha. ~ back kumbusha I was carried back to my youth nilikumbuka ujana wangu their courage will ~ them through ujasiri wao utawasaidia. n 1 (of a gun range) masafa. 2 uchukuzi, ubebaji. carrier n 1 mchukuzi common carrier uchukuzi wa aina yoyote; mpagazi; hamali; kampuni ichukuayo bidhaa. 2 aircraft carrier n manowari ya kuchukulia ndege (agh. za vita). 3 keria: kiungo cha chuma cha kuchukulia mizigo n.k. katika baiskeli au motokaa. 4 electric carrier n kipitisha umeme. 5 (biol) kichukuzi. 6 (of disease) mwenezaji. carrier-bag n mfuko wa karatasi au plastiki. carrier-pigeon n njiwa-kijumbe.