business

n 1 biashara; kufanya biashara he is in the timber ~ anafanya biashara ya mbao start a ~ anza biashara. ~ address n anwani ya biashara au ofisi. ~ hours n saa za kazi. ~ like adj -epesi; chapa kazi. -angalifu. ~ man n mfanyabiashara. 2 kazi, shughuli. on ~ -wa katika shughuli. I am here on ~ nipo hapa kwa shughuli. 3 kazi, wajibu, jambo linalopasa It is my ~ to advise you ni wajibu wangu kukushauri. get down to ~ anza kufanya kazi iliyokusudiwa. mind your own ~! si shauri lako! haikuhusu! mean~! jali, -wa makini. send somebody about his ~ fukuza na onya (mtu) asiingilie mambo. 4 madaraka; haki, you have no ~ to interfere usiniingilie. 5 jambo gumu, tatizo what a ~ it is tatizo gani hili. 6 jambo (la kukifu, kukera, kuchosha) I am sick of the whole ~ jambo hili limenikifu. 7 (colloq) the ~ end of a pin/a chisel etc ncha ya kitu/chombo (inayotumika kufanyia kazi). 8 (theatre) ishara za uso kuelezea, kufasili sehemu wanazoigiza (tofauti na wasemavyo). 9 like nobody's ~ vizuri/haraka sana.