buffer

n 1 bafa: kifaa kitumiwacho katika kupunguza athari ya nguvu ya msukumo wakati gari inapogonga kitu. ~ zone n eneo la amani. 2 kinga: kitu au mtu anayemkinga mtu mwingine au kitu kingine kisipate mshtuko. 3 (sl) old ~ n mtu aliyepitwa na wakati au mjinga. 4 sehemu ya hifadhi ya muda (hasa katika kompyuta). ~ state n taifa kati: taifa dogo lisilopendelea upande wowote ambalo liko kati ya mataifa mawili yaelekeayo kuchukiana. ~stock n akiba: hifadhi ya kitu inayonunuliwa wakati bei ni nafuu na kuwekwa ili itumiwe wakati bei yake itakapokuwa ghali. vt 1 punguza mshtuko; punguza athari ya mgongano. 2 zuia kupata maumivu.