buck

n 1 dume (la wanyama jamii ya paa, mbuzi, sungura, n.k.). 2 kifaa cha kuchezea sarakasi. 3 egemeo la mti wakati wa kupasua mbao. 4 mnyama aina ya paa (hupatikana zaidi Afrika Kusini). 5 (colloq) mtu wa miraba minne. 6 (US) dola; (arch) kijana maridadi. ~ fever n homa ya kutetemeka; wasiwasi unaomwingia mtu anapokabiliwa na jambo geni (k.m. anapoanza madaraka mapya anapokumbana na tatizo gumu n.k.). vi 1 (of horse/mule) ruka hewani na kutua chini kwa kutanguliza miguu ya mbele huku kichwa kimeinama. 2 enda au simama ghafla kwa mtikisiko au mshtuko. 3 gonga au gongana na kitu kwa ghafla. pass the ~ kwepa wajibu. ~ up 1 fanya haraka. 2 tia moyo. ~ skin n ngozi laini (k.m. ya paa/mbuzi) inayotumika kutengenezea glovu, mikoba n.k.). ~ short n aina ya risasi. ~ tooth n jino lililotokeza.